![]() |
| Waziri mkuuu mstaafu, fredrick sumaye |
Na Fredy Azzah, Masasi
.......................................WAZIRI Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, amesema ameanza kupata vitisho baada ya kuzungumza mambo mbalimbali ya Serikali katika kampeni za mgombea urais wa Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa.
Akizungumza jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Viwanja vya
Madeko, Jimbo la Ndanda wilayani Masasi mkoani Mtwara, Sumaye alisema
vitisho hivyo ni pamoja na kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,
Nape Nnauye aliyemtaka kunyamaza vinginevyo atamshughulikia.
“Anasema Sumaye anyamaze vinginevyo tutamshughulikia, sijui atanishughulikia kwa lipi, lakini ole wake nikipata tatizo lolote.
“Anasema Sumaye anyamaze vinginevyo tutamshughulikia, sijui atanishughulikia kwa lipi, lakini ole wake nikipata tatizo lolote.
“Nataka wapande jukwaani watuambie dawa za kulevya zinazokamatwa kila
siku magunia na magunia ni za nani na mpaka sasa amefanywa nini? Meno
ya tembo yanayokamatwa huko ni ya nani na mpaka sasa hivi kafanywa nini?
“Meli mbovu iliyopo Dar es Salaam ambayo sasa imeletwa Lindi ili
kuwadanganya wananchi, nani kainunua na kafanywa nini, mabehewa mabovu
nani kanunua na kachukuliwa hatua gani.
“Siyo nikisema haya unasema utanishughulikia, utanishughulikia we nani? Kama hawana majibu ya haya, lazima waondoke, ndiyo utaratibu duniani kote, wanashangaa nini?
“Kama hawataki kuondoka waseme kuwa wao ni madikteta tujue… Kama ni chama cha siasa kama vingine, Oktoba 25 wanaondoka asubuhi,” alisema Sumaye.
Sumaye alisema hali ya kutishwa haipo kwake pekee, bali hata kwa wananchi ambao wanadanganywa wakichagua upinzani nchi itakuwa na vita.
Alisema Libya, Misri ilipata machafuko, baada ya Serikali kukataa kusikiliza wananchi.

No comments:
Post a Comment