![]() |
Mgeni
rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues (wa pili kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja
wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan mara baada ya
kuwasili kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Nyanza jijini Mwanza kwenye
maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani ambapo kitaifa yamefanyika
jijini humo na kuandaliwa na Baraza la Dini mbalimbali la Amani Tanzania (IRCPT)
kwa ushirikiano wa UNESCO ambapo yaliwashirikisha Viongozi wa Serikali,
Asasi za Kiraia, Waandishi wa habari, Viongozi wa madhehebu ya dini,
Jeshi la Polisi, Walemavu, Wananchi pamoja na Ofisi ya Msajili wa vyama
vya siasa. Kushoto ni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis
Mutungi na wa pili kulia ni Afisa Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya
siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick Ringia. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog). |
……………………….
Na Modewjiblog team, Mwanza
Umoja
wa Mataifa (UN) umesema utaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania
kulinda na kudumisha amani ya pamoja kwa makundi yote ili amani iliyopo
itumike kuleta maendeleo endelevu nchini.
Hayo
yamebainishwa na Mgeni rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),
Zulmira Rodrigues, wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya
siku ya Amani Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza (Septemba
21.2015).
Bi.Rodgrigues
amesema amani ya pamoja inatoa nafasi kwa kila mmoja kuwa mshirika wa
kudumisha na kuendeleza amani bila kujali itikadi, imani au matabaka
mbalimbali yaliyipo ndani ya jamii.
Amefafanua
kuwa Tanzania ni mfano wa kuigwa katika kulinda amani, hivyo nguvu ya
pamoja ni muhimu katika kufikia malengo na maendeleo yanayotakiwa
kutokana na kuwepo kwa utulivu, mshikamano, umoja, na amani.
Kwa upande wake, Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amewataka watanzania kuachana na propaganda za kisiasa zinazoleta chuki na hasa katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Jaji
Mutungi ameeleza kuwa amani haina tabaka na kusisitiza umuhimu wa
wananchi kupiga kura kwa kutumia falsafa ya kulipenda taifa na kuwaonya
viongozi wa vyama vya siasa kuacha kuwadharau watanzania ambao
wameilinda amani kwa muda mrefu.
Nalo
Jeshi la Polisi mkoani humo, limelaani kitendo kilichofanywa na watu
wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa vyama vya siasa kwa kushambulia polisi
na kuvunja vioo vya gari la polisi kwa kusingizio cha kampeni za
uchaguzi.
Katika
tukio hilo imeelezwa kuwa, baada ya watu waliokuwa wakitokea katika
mkutano wa kampeni wa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) kushambulia
Polisi, kuvunja vioo vya gari la polisi na kujeruhi askari.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo
ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika
kilele hicho cha siku ya Amani jijini hapa.
Kamanda Mkumbo ameeleza kuwa kitendo hicho ni uhalifu kama uhalifu mwingine na polisi haiwezi kuvumilia vitendo vya aina hiyo na hasa wakati huu ambapo kampeni za uchaguzi zinaendelea.
Maadhimisho
ya siku ya amani duniani yanafanyika septemba 21, kila mwaka ili
kukumbuka na kulinda amani na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Amani Kwanza –
Utamaduni wetu wa amani ni nguvu yetu”.
Ambapo siku hiyo pia viongozi
mbalimbali waliweza kuhudhuria siku hiyo wakiwemo viongozi wa siasa,
dini, jeshi la Polisi, viongozi wa serikali na binafsi pamoja na
wananchi mbalimbali.
![]() |
Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Amani Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Mwanza. |
![]() |
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi akitoa nasaha zake kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani Duniani ambapo kitaifa yamefanyika jijini Mwanza. |
![]() |
Jukwaa kuu la viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani ambapo kitaifa imefanyika jijini Mwanza. |
![]() |
Kikundi cha kwaya ya Patimo-Mabatini jijini Mwanza kikitoa burudani kwenye maadhimisho hayo. |
![]() |
Burudani ya Qaswida maalum iliyobeba ujumbe wa kutunza ‘Amani’ ikitolewa. |
![]() |
Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo (kushoto) na viongozi mbalimbali wa dini wakiendelea kusaini Azimio hilo. |
![]() |
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi naye akiweka saini kama shuhuda wa kupitisha Azimio hilo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Baraka Konisaga. |
![]() |
Wawakilishi wa vikundi vya vijana walioshiriki maadhimisho ya siku ya Amani Duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Mwanza. |
![]() |
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya msingi Nyanza walikuwa ni miongoni mwa washiriki wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani duniani. |
![]() |
Meza kuu katika picha ya pamoja. |
![]() |
Washiriki katika picha ya pamoja. |
No comments:
Post a Comment