![]() |
Jeneral Gilbert Diendere |
Jenerali Gilbert
Diendere aliyefanya mapinduzi nchini Burkina Faso amesema kuwa yupo
tayari kukabidhi serikali kwa utawala wa kiraia kama ilivyopendekezwa na
wapatanishi.
Diendere ambaye alipindua serikali hiyo siku ya
alhamisi wiki iliyopita anasema kuwa alifikia uamuzi huo kwa lengo la
kile anachokiita kuepusha umwagaji mkubwa wa damu.
Kauli yakekukiri kukabidhi madaraka inakuja huku majeshi ya serikali yaki ukaribia mji mkuu wa Ouagadougou
Jeshi
la Burkina Faso limeahidi kuwepo kwa hali ya Usalama kutokana na
mapinduzi hayo,japo kuwa wameahidi kuto waangamiza waliofanya mapinduzi
hayo iwapo tu watasalimisha silaha zao.
Hata hivyo kwa sasa Jeneral Diendere anadaiwa kujificha nyumbani kwa kiongozi wa kijadi Mogho Naaba.
Mamia ya watu wamezagaa mitaani katika mji mkuu wa nchi hiyo kwaajili ya kusherehekea.
No comments:
Post a Comment