………………………………..
Na Mwandishi Wetu
WADAU wa Michezo mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kujitokeza
kuisaidia Serikali kukuza michezo na kufufua vipaji vya wachezaji katika
fani mbalimbali katika shule za msingi na Sekondari.
Akizungumza katika sherehe ya kuwapongeza wachezaji na wadau
mbalimbali walioshiriki michezo ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule
za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) Dar es Salaam juzi,Kaimu Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Raymond Mushi aliwataka wadau wa michezo kujitokeza
kusaidia Serikali kufufua vipaji vya wachezaji kutoka ngazi ya shule ya
msingi na sekondari.
Mushi alimpongeza Rais Jakaya
Kikwete anayemaliza muda wake kurudisha michezo hiyo mashuleni baada ya
kuondolewa katika uongozi wa RAis Mpaka hivyo kuathiri vipaji vya vijana
wengi kushindwa kung’ara katika medani ya michezo nchini.
Katika sherehe hizo ambazo mkoa
wa mkoa wa Dar es Salaam waliokuwa ukipongezwa kwa kutwaa ubingwa wa
jumla za mashindano hayo yaliyofanyika mkoa wa Mwanza mapema mwaka
huu,Meneja wa timu ya UMITASHUMTA ya Mkoa wa Dar es Salaam, Adolf Ally
alisema haikuwa rahisi kupata ushindi huo kwa sababu mikoa mingi
ilidhamiria kupata ushindi huo lakini wao walijiandaa zaidi kwa
kushirikiana na wadau.
Mkurugenzi wa MAsoko wa Kampuni ya Isere Sports, Abbas Ally
ambao ni wauzaji wa vifaa michezo nchini aliyepata tuzo ya wadau
waliofanikisha kupatikana kwa ushindi huo aliahidi kuongeza vifaa vyenye
ubora kwa bei nafuu ili mwakani mkoa huo uendelee kuwa mabingwa.
Aliwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia michezo ili
kurejesha hadhi ya michezo katika shule za msingi na Sekondari ili
kujenga timu imara za Ligi Kuu na timu ya Taifa ya Tanmzania (Taifa
Stars).
Mkoa wa Dar es Salaam uliochukua ushindi wa jumla kwa kutwaa
medali 26 katika michezo mbalimbali lakini ikiwemo soka ya wanawake
lakini ilijikuta inafungwa katika mchezo wa soka ya wamaume baada ya
kupachikwa bao 1-0 na wenyeji Mwanza.
No comments:
Post a Comment