![]() |
LIVERPOOL, ENGLAND
BAADA ya Liverpool kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Norwich City, mashabiki wamemtaka bosi wa klabu hiyo kumfukuza
kocha wao Brendan Rodgers. Klabu hiyo mpaka sasa imefanikiwa kushinda michezo miwili kati ya sita iliyocheza
huku ikitoa sare miwili na kufungwa miwili.
kocha wao Brendan Rodgers. Klabu hiyo mpaka sasa imefanikiwa kushinda michezo miwili kati ya sita iliyocheza
huku ikitoa sare miwili na kufungwa miwili.
Katika mchezo wa jana Liverpool ilikuwa nyumbani na kutoka sare dhidi
ya klabu ambayo imepanda daraja msimu huu, hivyo mashabiki wa klabu
hiyo wamemtumia ujumbe bosi wa klabu hiyo John Henry, kupitia
akaunti yake ya Twitter.
Wengi wamesema wakati wa Rodgers kuifundisha klabu hiyo umekwisha na
huu ni wakati wa kutafuta kocha mwingine wa kuweza kuchukua nafasi hiyo.
Hata hivyo, kutokana na malalamiko ya mashabiki, inasemekana kuwa
tayari uongozi wa klabu hiyo umefanya mazungumzo na kocha wa klabu ya
Dotmund ya nchini Ujerumani, Jurgen Klopp na kocha wa zamani wa
klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti.
klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti.
kutokana na matokeo hayo mabaya, kocha huyo amewataka wachezaji
wake kujituma zaidi ili kurudisha heshima ya klabu hiyo katika uwanja wa
nyumbani.
“Ni kweli tumefanya vibaya katika michezo yetu, lakini ni wakati sasa
wa kubadilisha matokeo katika michezo ijayo ili kuweza kurudisha
heshima ya Uwanja wa Anfield.
“Anfield ni sehemu pekee ya sisi kuonesha uwezo wetu kisoka, tunatakiwa kuutumia vizuri uwanja wetu ili kuwapa
nguvu mashabiki ambao wanajitokeza uwanjani.
nguvu mashabiki ambao wanajitokeza uwanjani.
“Kwa upande wangu najisikia vibaya na matokeo ambayo tumeyapata,
lakini ninaamini tuna kila sababu ya kubadilika na kufanya kile ambacho
klabu inataka,” alisema Rodgers.
No comments:
Post a Comment