KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 4, 2015

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI WA MKOA WA MTWARA CHAENDESHA ZOEZI LA USAFI NA KUPANDA MITI KATIKA HOSPITALI YA MKOA HUO

Displaying 004.MTWARA.jpg
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Halima Dendego(kushoto) akiwashuhudia vijana walioadhirika na madawa ya kulevya wa mkoa huo wakiuweka mti sawa mara baada ya Mkuu wa Mkoa huo kuupanda mti huo wakati wa shughuli maalumu ya kufanya usafi na kupanda miti(10)katika hospitali ya mkoa huo iliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari wa mkoa huo na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Displaying 002.MTWARA.jpg
.Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Halima Dendego(wapili toka kushoto)akiambatana na Mkuu wa Wilaya Mtwara,Fatma Ally pamoja na Meneja uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(kulia)na  baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwasili katika hospitali ya Mkoa wa Mtwara katika kushirikiana na Chama cha waandishi wa habari cha mkoa huo na vijana walioadhitika na madawa ya kulevya mkoani humo kufanya usafi na kupanda miti kuzunguka hospitali hiyo.
Displaying 001.MTWARA.jpg
Mwandishi wa habari wa Mwananchi Communication,Haika Kimaro(kushoto) pamoja na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu wakishiriki kufanya usafi katika hospitali ya mkoa wa Mtwara. Ambapo chama cha waandishi wa habari cha mkoa huo kwa kushirikia na Vodacom Tanzania na vijana waliohadhirika na madawa ya kulevya vilianda shughuli hiyo na kupanda miti 10 kuzunguka hospitali hiyo.

Displaying 003.MTWARA.jpg
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Halima Dendego(wapili toka kushoto) na Mkuu wa Wilaya Mtwara,Fatma Ally pamoja na Meneja uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(kushoto)na  baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa mtwara na vijana walioadhirika na madawa ya kulevya wa mkoa huo wakishiriki katika zoezi la kufanya usafi katika hospitali ya mkoa wa mtwara.Shughuli hiyo iliandaliwa na chama cha waandishi wa habari wa mkoa huo na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

No comments:

Post a Comment