Napenda
kuchukua nafasi hii kwa masikitiko kutuma salamu za rambirambi kwa
Familia pamoja na wanachama wa Chama cha DP (Democratic Party) kufuatia
kifo cha Mchungaji Christopher Mtikila kilichotokea asubuhi ya leo
tarehe 4 Oktoba 2015. Kwa niaba ya wenzangu katika CHADEMA na UKAWA na
kwa niaba ya familia yangu, ninamwomba Mwenyezi Mungu awape faraja
wafiwa na amweke Marehemu mahala pema.
Bwana Ametoa. Bwana Ametwaa. Jina Lake Lihimidiwe.
Bwana Ametoa. Bwana Ametwaa. Jina Lake Lihimidiwe.
No comments:
Post a Comment