Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya sherehe za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa pamoja na kutolea ufafanuzi malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) yenye lengo la kufuta kabisa umaskini.(Picha zote ne Geofrey Adroph wa Pamoja Blog). |
Baadhi ya Maofisa wa Umoja wa Mataifa na maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiendelea kufuatilia yanayojiri kwenye mkutanoni na waandishi wa habari. |
Waandishi wa habari wakifuatilia kinachoendelea mkutanoni. |
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) wakiwa wameshikilia lengo namba 1 na 13 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia. |
Mwanafunzi wa shule ya msingi ya Agha Khan, Iman Kawambwa akiwa ameshikilia lengo namba 4 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia. |
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa wameshikilia lengo namba 5 na 10 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia. |
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akiwa ameshikilia lengo namba 17 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia. |
Afisa Habari wa Shirika la kazi duniani (ILO) Tanzania, Magnus Minja na Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo wakiwakilisha lengo namba 1 na 8.n |
Baadhi ya wandishi wa habari wakiwa wameshika namba mbalimbali za malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia. |
…………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Kila Oktoba 24 ya kila mwaka,
Umoja wa Mataifa huadhimisha siku ya kuundwa kwake. Kwa mwaka huu
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania yanayofanya kazi kama
taasisi moja yameendelea kujishughulisha na kazi mbalimbali za kijamii
zenye lengo la kuadhimisha miaka 70 ya kuundwa kwa umoja huo.
Akizungumza na waandishi wa
habari Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa
UNDP Bw. Alvaro Rodriguez kuhusu umuhimu wa malengo hayo amesema “Kwa
hakika maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa ni wito wa
kujitazama, kuona yale tuliyofanya kwa miongo kadhaa na kujikita kuona
namna ya kuabiliana na umaskini hapa nchini Tanzania na Duniani kwa
ujumla.
“Malengo ya Maendeleo endelevu
ni wito wa kuwajibika kwetu sote. Hakuna mtu anayeweza kufanikiwa akiwa
peke yake. Inabidi tufanye kazi kwa pamoja,wadau wote,serikali na bunge,
vyama vya kiraia, madhehebu ya kidini, wafanya biashara, wajasiliamali,
na wanazuoni.
Na hakika tukishirikiana kwa nguvu pamoja na amani
tunaweza kufikia malengo ya maendeleo endelevu”.
Pia alisistiza kuwa “Malengo ya
dunia yaliyojengwa katika Malengo ya Milenia yamelenga kukabiliana na
matatizo ya zamani kwa mbinu mpya.
Zimelenga kukabiliana na tatizo
la umaskini na ukosefu wa usawa katika masuala ya uchumi. SDGs haiwezi
kufanikiwa bila kuyaangalia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, usawa
wa jinsia, haki za biandamu na kukabiliana na mfumo inayobagua.”
Akizungumzana waandishi wa
habari Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya amesema kuwa nia ya
serikali ni kuendelea kushirikiana na mashirika ya umoja wa mataifa na
kuwatakawatengeneze sera nzuri ambazio zitahakikisha hakuna mtu
anayeachwa nyuma katika mipango ya maendeleo ya kitaifa.
Aliendelea kufafanua kwa kusema
Tanzania inafurahishwa na ukweli unaoonekana kwenye malengo mapya ya
maendeleo endelevu kwani yamechota pia yale malengo ya milenia ambayo
yalikuwa bado hayajamaliziwa kwani katika hayo kunaweza kuleta
mabadiliko ya kuwezesha kuondokanana umaskini katika sura zake zote
ifikapo mwaka 2030.
Maadhimisho ya Umoja wa mataifa
yatafavyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam siku ya
Jumanne Oktoba 13 badala ya siku iliyozoelekaya Oktoba 24 ili kupisha
uchaguzi mkuu wa Tanzania unaofanyika Oktoba 25.
Na kauli mbiu ya
maadhimisho ya Umoja wa mataifa mwaka huu ni “Umoja wa Mataifa
uliothabiti, Dunia bora”.
No comments:
Post a Comment