![]() |
Wakati
waswahili wanasema adui yako mwombee njaa, msemo huo umekuwa tofauti
kwa upande wa mgombea ubunge wa ACT - Wazalendo Jimbo la Arusha Mjini,
Estomih Malla baada ya jana kupanda jukwaani na kumwombea kura za ndiyo
mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.
Mgombea
huyo alikuwa akihutubia mkutano wa kampeni uliokuwa na lengo la kunadi
pia sera na kumwombea kura mgombea wa chama chake, Anna Mnghwira, katika
Uwanja wa Stendi Kubwa, mkoani hapa.
“Jamani
naombeni mtambue kuwa mimi ni msomi ambaye nina shahada (Hakuitaja ni
ya nini), kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikitumia elimu yangu kwa faida
ya familia yangu tu baada ya kufukuzwa udiwani na Chadema, sasa naombeni
mnichague ili niitumie pia kuwatumikia kwa kuwaletea maendeleo
yaliyoshindikana kupatikana kwa miaka mitano,” alisema.
Mgombea huyo, alisema maendeleo ya kweli yanaletwa na watu wa kweli na wazalendo. “Mimi
ni mkweli, nipeni ridhaa ya kuwaongoza na msisahau kumpa ridhaa ya kuwa
rais mheshimiwa Edward Lowassa, naamini hamtajutia kura zenu,” alisema Malla.
Alipoulizwa
baada ya kumaliza mkutano wake kwa nini amemnadi Lowassa badala ya
mgombea urais wa chama chake, Malla hakutaka kujibu bali alipanda gari
lake na kuondoka.
No comments:
Post a Comment