KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 6, 2015

MKUTANO WA PILI WA MWAKA WA KIMATAIFA WA WATAALAM WA KUDHIBITI MBU WAFUNGULIWA RASMI DAR ES SALAAM

MKURUGENZI  Mkuu wa Taasisi ya Utafiti  wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI), Dk.
Mwele Malecela akifungua mkutano huo wa pili wa mwaka wa kimataifa wa wataalam
wa kudhibiti Mbumbu kwa Nchi zisizofungamana Afrika (PAMCA) ulioanza  jijini
Dar es Salaam Oktoba 6, 2015.
Mapema akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa  Kimadawa Kenya (KEMRI), Musau Kyanesa amesema
lengo la kuanzishwa kwa PAMCA ni kutafuta njia stahiki ya kupambambana na mdudu
mbu ambae hueneza magonjwa mbalimbali ambayo huathiri binadamu.
“Itakuwa ni jambo jema sana kama tutaweza kumdhibiti mdudu huyu mbu ambaye anaeneza
magonjwa haya na kufanikiwa kwa hilo tutaweza kuendeleza afya za wananchi wetu
kwa nchi za Afrika, maana Afrika ndio tunapata shida sana na mdudu huyu mbu,”
alisema Kyanesa.
Aidha Kyanesa ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa KEMRI amesema wameandaa mpango wa kuhamasisha wanafunzi vyuoni kujikita katika sayansi ya Mbu ili kupata watalaam wengi wakuweza kukabiliana mbu Kenya na Afrika kwa ujumla. 
“Tunaandaa mpango wa kuhamasisha vijana kusomea na hatimaye kuwa na utaalm juu ya mapambano na kufanya tafiti za mbu, kwa kugharamia masomo yao kutokana na upungufu wa wataalam kulingana na tatizo lenyewe,”alisema Kyanesa.

Mwenyekiti wa Bodi ya PAMCA, Prof Charles Mbogo akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo.
 
 Washiriki wakisikiliza mada mbalimbali katika siku ya kwanza ya mkutano huo, Dar es Salaam leo.
Rais wa PAMCA tawi la Tanzania, Dk Stephen Magesa akizungumza katika mkutano huo.
 
Mkuu wa NIMRI Tanzania, Dk. Mwele Malecela akizungumza na Mkurugenzi Msaidizi wa KEMRI kutoka Kenya, Musau Kyanesa baada ya ufunguzi wa mkutano huo.
Prof Wen Kilama akiwasilisha mada juu ya Maadili ya Utafiti wa Afya hususani Maleria Afrika .
Prof Wen Kilama akiendelea na uwasilishaji wa mada yake. Prof Kilama ni Mkurugenzi Mstaafu wa NIMR.
 Dk Mwele Malecela na washiriki wengine wakifuatilia mada ya Prf Kilama.
 Washiriki wakifuatilia mada hiyo.
Picha ya pamoja ya washiriki mkutano huo wakiwa na mgeni rasmi.

No comments:

Post a Comment