Kocha
mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia
ya Kilimanjaro, Charles Mkwasa amesema kikosi chake kipo tayari kwa
mchezo wa kesho dhidi ya Malawi kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la
Dunia mwaka 2018.
Mkwasa amesema kikosi chake kipo
kaika hali nzuri baada ya kufanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi ambapo
wachezaji wote wapo katika hali nzuri wakiwemo wachezaji wawili Mbwana
Samata na Thomas Ulimwengu kutoka klabu ya TP Mazembe ya Congo DR.
“Tunatambua umuhimu wa mchezo wa
kesho, wachezaji wana ari na morali ya hali ya juu, kikubwa tunawaomba
watanzania wajitokeze kwa wingi uwanjani kuja kutu sapoti katika mchezo
huo wa kesho” Alisema Mkwasa.
Kwa upande wa kocha msaidizi wa
Malawi (The Flames), Ramadhan Nsanzurwimo amesema wanaiheshimu Tanzania,
wanatambua kesho kutakua na mchezo mzuri, na wao kama Malawi
wamejiandaa vizuri kwa mchezo huo.
No comments:
Post a Comment