Waziri mkuu wa jimbo la Bihar nchini
India ,Nitish Kumar (pichani) ametangaza mipango ya kupiga marufuku uuzaji na
utumizi wa pombe katika jimbo hilo.Hatua hiyo italigharimu jimbo la Bihar zaidi ya dola milioni 500 za kodi,kulingana na msemaji wa chama tawala cha Bihar Janata Dal.
Pombe imepigwa marufuku katika majimbo kadhaa ya India ikiwemo Gujarat na Manipur.
Bwana Kumar anaongoza muungano wa vyama vya kijimbo vilivyochukua mamlaka katika jimbo la Bihar mapema mwezi huu.
Wakati wa kampeni zake,alikabiliwa na maandamano ya wanawake ambao walilalama kuhusu ubugiaji mbaya wa pombe katika vijiji.


No comments:
Post a Comment