![]() |
Kikosi cha timu ya taifa ya
Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ kinatarajiwa kuwasili kesho mchana
jijini Dar ess alaam kikitokea nchini Ethiopia kilipokuwa kinashiriki
michuano ya Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati. Kilimanjaro Stars imetolewa katika hatua ya robo fainali na wenyeji Ethiopia kwa mikwaju ya penati, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za mchezo huo, na wenyeji kushinda kwa penati 4-3. Timu ya Kilimanjaro Stars inayonolewa na kocha Abdallah Kibadeni na msaidizi wake Juma Mgunda, iliongoza kundi lake katika hatua ya makundi kabla ya kukutana na wenyeji Ethiopia katika mchezo wa robo fainali. Katika michezo wa makundi, Kilimanjaro iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Somalia, ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Rwanda, na sare ya bao 1-1 dhidi ya Ethiopia. Baada ya kurejea nyumbani, TFF kwa kushirikiana na benchi la ufundi wataanza maandalizi ya michezo dhidi ya Chad itakayochezwa Machi 2016 kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2017. |
December 1, 2015
KILIMANJARO STARS KUREJE KESHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment