KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

December 3, 2015

MABONDIA THOMASI MASHALI NA FRANSIC CHEKA WATAMBIANA KUZIDUNDA DESEMBA 25 MOROGORO

Mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka wakitunishiana misuli wakati wa kutambulisha mpambano wao utakaofanyika katika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro Desemba 25 


Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Thomas Mashali wa Dar es salaam na Fransis Cheka wa Morogoro wamendelea kutambiana kuelekea mpambano wao wa Desemba 25 utakaofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro uzito wa kg 76
Akiongea na waandishi wa habari Mashali amesema kuwa hii ni vita ya Dar na Moro  hivyo kawaomba wapenzi wa mchezo wa masumbwi wa Dar es salaam waweze kuhamia morogoro kwa muda kwa ajili ya kumsapoti
Siku hiyo ambayo kwake atakuwa na kibaruwa kigumu ambapo atapigana na Cheka pamoja na wakazi wa Morogoro
Naye Cheka alijibu mapigo hayo kwa kusema siku zote anamweshimu bondia anaetaka mpambano wa marudiano hata hivyo dozi ya mashali ipo pale pale na nitampiga katika raundi za awali tu kwa kuwa yupo  vizuri na naendelea na mazoezi
  Kocha wa Mashali Ramadhani Uhadi amesema kuwa Cheka ni bondia wa kawaida sana hivyo wapenzi waje waone mchezo mzuri utakaochezwa na Mashali atakavyo msambalatisha Cheka siku hiyo mjini Morogoro
Naye kocha wa bondia Cheka Abdallah Salehe amesema Cheka yupo vizuri sana kwa sasa nimempika ameshaiva ata kama mpambano utakuwa leo Mashali atapigwa mapema sana
Katika mpambano huo kutakuwa na mipambano mingine ya bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' atapambana na Twaha Kassimu kg 63 na Vicent Mbilinyi kg 63 atakumbana na Deo Njiku wakati Pius Kazaula kg 66 atamenyana na Seba Temba mpambano mwingine utawakutanisha mabondia Epson John  kg 57 na Sadiq Momba na wana dada Lulu Kayage kg 51 atapambana na Mwanne Haji kugombania ubingwa wa taifa.

No comments:

Post a Comment