![]() |
Profesa Ibrahim Lipumba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CUF na aliyekuwa akikabiliwa na kesi pamoja na wafuasi 30 wa CUF katika
Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam akidaiwa kufanya
mkusanyiko bila ya kuwa na kibali cha Polisi, amefutiwa mashitaka na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Kesi hiyo imefutwa rasmi leo baada ya DPP kuileleza mahakama kuwa hana nia tena ya kuendelea na kesi hiyo.
Lipumba alijiweka kando na CUF baada ya Umoja wa Ukawa kumkaribisha Edward Lowassa kugombea nafasi ya Urais kwa tiketi ya Chadema, haya hiyo katika Uchaguzi huo, Dkt.John Pombe Magufuli aliibuka kidedea.
|
December 3, 2015
BREAKING NEWS: PROFESA LIPUMBA AFUTIWA KESI LEO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment