Desemba 2.2015:Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo imezindua huduma mpya inayojulikana kama
Vodacom Red ambayo imewalenga wateja wake wote wanaonunua
muda wa maongezi kabla ya kupata huduma za mawasiliano ambayo ni bora
zaidi,ina unafuu wa gharama na yenye kuwarahishia maisha.
Akiongea
wakati wa uzinduzi jijini Dar es Salaam leo,Mkurugenzi Mtendaji wa
Vodacom Tanzania,Ian Ferrao amesema“Vodacom tumebuni huduma tukiwa
tumewalenga wateja wetu wote hasa wale wenye shughuli nyingi ambao
wanakosa muda wa kununua vifurushi vya muda wa maongezi vya siku,wiki
na vya mwezi.Huduma ya Vodacom Red itawapatia unafuu wa kupiga simu kwa
mitandao yote kwa gharama ya shilingi 1.5 kwa
sekunde na kwa gharama hiyo hiyo ya shilingi 1.5 kwa sekunde
watawezeshwa kupiga simu katika nchi tano kubwa zenye mtandao mkubwa wa
masuala ya biashara ambazo ni (China,Afrika ya Kusini,India,Canada na
Marekani),Kuhusiana na matumizi ya data alisema wateja
watakaotumia huduma hii watapatiwa kifurushi chenye unafuu
kitakachowawezesha kupata huduma za intaneti yenye kukidhi mahitaji
yao” .
Kampeni
hii inawarahisishia maisha watumiaji wake kwa kutoa ofa kwa watumiaji
ambapo watafanya mawasiliano kwa kupiga simu za ndani
kwa malipo nafuu ya shilingi 1.5 kwa sekunde kwa mitandao yote pia kwa
gharama hiyo hiyo ya shilingi 1.5 wanaweza kupiga simu kwenda nje ya
nchi zipatazo 5 pia wanaunganishwa na huduma ya intaneti ya Mpango Mzima
ambayo ina kasi kubwa na inawawezesha kufanya
kazi zao kwa ufanisi kwa muda wote.Katika kusherehekea uzinduzi wa
huduma hii wateja watakaotumia shilingi 4,000/-na zaidi kwa kupiga simu
za ndani watanufaika na mrejesho wa asilimia 10% ya fedha hizo kupitia
akaunti zao za M-Pesa kwenye simu zao.
Akiongelea
mkakati wa Vodacom kuwaunganisha watanzania wote katika mtandao wa
mawasiliano,Ferrao alisema “Lengo letu ni kuendelea kubuni
huduma za kurahisisha mawasiliano kwa wateja wetu tukiwa na dhamira ya
kuwapeleka katika ulimwengu wa sayansi na
teknolojia.Vodacom Red ni mfano wa
huduma ambayo imebuniwa ikiwa ina ufanisi kubwa katika masuala ya
biashara na yenye kuleta unafuu wakati huohuo kuwarahisishia maisha
wateja wetu”.
Wateja
wa Vodacom wanaotumia huduma ya kuongeza salio kwenye simu zao kabla ya
maongezi wanaweza kuchangamkia huduma mpya na yenye unafuu
mkubwa wa gharama.Ili mteja aweze kunifaika na huduma hii anachotakiwa
kufanya ni kupiga *149*73# hapo mteja utapata frusa ya kuchagua
anachokitaka kupitia huduma ya Vodacom Red.
Mwisho.


No comments:
Post a Comment