JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTATUZI WA MGOGORO WA WAKULIMA WA MIWA KILOMBERO Bodi
ya Sukari Tanzania imefuatilia na kubaini chanzo cha malalamiko ya
wakulima wa miwa wanaozunguka Kiwanda cha Sukari cha Kilombelo (ILOVO).
Akizungumza
katika taarifa yake, Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Sukari Tanzania Bwana
Henry Semwanza alisema kuwa, chanzo cha malalamiko yanatokana na kiwanda
kuharibika bila kutarajia na kusimamisha uzalishaji kuanzia tarehe 14
hadi 18 Novemba 2015.
Hali
hiyo ilisababisha miwa ya wakulima ambayo ilikuwa imekatwa kuharibika
na hivyo kukosa sifa ya kuchukuliwa na kiwanda kwa ajili ya usindikaji.
Bwana
Semwanza aliongeza kuwa hali hiyo ilisababisha tani 250 za miwa
kutoruhusiwa kuingia kiwandani kwa vile zilishapita zaidi ya siku tano
tangu miwa ilipochomwa.
“Miwa
hiyo ilichomwa tangu tarehe 14 Novemba 2015 siku ambayo kiwanda
kiliharibika, na kilipotengamaa zilikuwa zimeshapita siku tisa, hivyo
miwa hiyo kukosa sifa na ubora unaokubalika, na hivyo ikazuiliwa kuingia
kiwandani”
Akizungumzia
utekelezaji wa mkataba wa ugavi wa miwa baina ya Kampuni na Vyama vya
Wakulima, Bwana Semwanza alibainisha kuwa Kifungu cha 5.2.3.3 cha
mkataba huo kinasisitiza kutokuikubali miwa ambayo kiwango cha ubora
wake uko chini ya asilimia 80 au miwa iliyopitisha siku tano tangu
ilipochomwa kwa mujibu wa kifungu cha 5.2.3.4.
Ili
kupunguza hasara inayoweza kutokea kwa wakulima, Bwana Semwanza
aliwakumbusha wakulima na wamiliki wa kiwanda kuzingatia taratibu za
uvunaji wa miwa.
“ninatoa
wito kwa wakulima kupitia vyama vyao kuzingatia taratibu za uvunaji
kwakuwa imedhihirika pasipo shaka kuwa baadhi wamekuwa wanavuna miwa
mingi zaidi ya mgao wao wa siku, mambo haya yasipozingatiwa yanaweza
kuibua migogoro isiyo ya lazima ” Bwana Semwanza alibainisha katika
taarifa yake.
Aidha,
alisisitiza kuwa kamati iliyoundwa chini ya mkataba wa ugavi wa miwa
inayojumuisha wakulima na uongozi wa Kiwanda na ambayo hukutana kila
siku iendelee kuwa msingi wa kuamua kiasi cha miwa inayotakiwa kuvunwa
na kupelekwa kiwandani katika siku inayofuata. Semwanza
aliongeza kuwa Bodi yake inaendelea kufuatilia utekelezaji wa
makubaliano kati ya kiwanda na wakulima, na haitasita kuchukua hatua
sitahiki kwa upande utakao kiuka ili kutatua migogoro inayoweza
kuzuilika kwa haraka.
Semwanza
alisisitza kuwa kwa sasa hali ni shwali ambapo uvunaji na upokeaji wa
miwa kiwandani unaendelea kama kawaida na wakulima wameongezewa mgawo wa
miwa inayotakiwa kuingizwa kiwandani kila siku.
“hali
ya uvunaji inaendelea kama kawaida na mgao wa wakulima kuingiza miwa
yao kiwandani umeongezwa kwa zaidi ya asilimia 50; ili kuhakikisha miwa
yote ya wakulima wanaozunguka kiwanda cha Kilombero inavuwa” Bodi
ya Sukari Tanzania inashirikiana kwa karibu na uongozi wa mkoa na
Wilaya ili kushughulikia migogoro isiyo ya lazima. Alihitimisha Bwana
Semwanza.
Imetolewa na:Kitengo cha Mawasiliano ya SerikaliWizara ya Kilimo Chakula
No comments:
Post a Comment