KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 7, 2016

JESHI LA UGANDA LATEGUA BOMU..,


Jeshi la Uganda UPDF na  polisi wakifanya doria katika mji mkuu Kampala  Uganda.
 Maafisa wa usalama nchini Uganda wametegua kifaa kinachoaminika kuwa ni bomu, kilichokuwa kimetegwa kwenye kituo cha  mabasi kaskazini mwa nchi hiyo kwenye mji wa Gulu karibu  na mpaka na  Sudan kusini....,

Raia waligundua kifaa hicho Jumatatu mchana   na kuwaita polisi pamoja na wanajeshi walikitegua kwa haraka bila kukikagua wakisema kwamba kilikuwa karibu kulipuka.

 Wapelelezi nchini humo wanaendelea na uchunguzi wao wakisema  kwamba  mabaki ya vifaa yamepelekwa maabara kwa uchunguzi zaidi na kuwatafuta wahusika  waliotega kifaa hicho kinachoaminika kama kingelipuka kingeweza kujeruhi au kuuwa watu walio mita hamsini za mraba kutoka pale kilipokuwa.

Mji wa Gulu unaopakana na Sudan Kusini ulishuhudia umwagikaji mkubwa wa damu wakati wa vita  vilivyoongozwa na kundi la waasi la Lord’s Resisitance Army linaloongozwa na Joseph Kony.

No comments:

Post a Comment