
Mwanasoka raia wa Tanzania anayechezea
TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mmbwana Ally
Samatta amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anachezea ndani ya
bara la Afrika, wakati tuzo ya mwanasoka bora barani Afrika ikienda kwa
Pierre-Emerick raia wa Gabon anayesakata kabumbumbu katika klabu ya
Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Tuzo hizo za kila mwaka zinazotolewa na Shirikisho la soka barani
Afrika almaarufu kama CAF zimetolewa usiku kuamkia leo mjini Abuja
nchini Nigeria. Kwa upande wa timu ya wanawake ya mwaka tuzo imekwenda
kwa timu ya Cameroon. Timu bora kwa wanaume kwa mwaka uliopita ni kutoka
Ivory Coast.
Kocha bora wa mwaka ni – Herve Renard,
kutoka Cote d’Ivore ambayo inashinda kwa mwaka wa pili mfululizo
wakati Klabu bora ya soka barani Afrika ni – TP Mezembe, kutoka DR Congo
ambapo mwanasoka bora wa kike Afrika ni Gaelle Enganamouit kutoka
Cameroon na Mwamuzi bora wa mwaka ni – Bakary Gassama kutoka nchini
Gambia.
No comments:
Post a Comment