KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 7, 2016

TANZANIA KUTIMUA WAHAMIAJI HARAMU

 Tanzania imeanzisha  zoezi la kufukuza wageni wanaofanya kazi nchini humo kinyume cha sheria. 

Wafanyakazi wengi wa kigeni haswa wale wa nchi za jirani,wataathiriwa na uamuzi huo kwani ni vigumu na ghali kupata hati ya muda mrefu ya kufanyia kazi.

Ofisi ya Uhamiaji ya Dar es salaam  imesema wanatambua kuwa kuna wahamiaji 350 walioko Jijini Dar es salaam wanaofanya kazi au kufanya biashara bila hati halali  kuanzia kwenye maduka makubwa ya Tanzania-Soko la Kariakoo hadi kwenye shule za watu binafsi,Ofisa uhamiaji John Msumule amesema kwamba  uchunguzi wao wamegundua kwamba wahamiaji wengi wanakuja nchini kwa viza ya utalii  na kuishia kufanya biashara kinyume na sheria  ndani ya nchi.

Shule nyingi za watu binafsi wanaajiri walimu kutoka nchi jirani kama Kenya na Uganda.BBC

4 comments: