Waziri wa Maliasili na Utalii Mh.
Profesa Jumanne Maghembe akizungumza na Menejimenti ya Bodi ya Utalii
leo jijini Dar es salaam.
Kamimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa
Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi akitoa taarifa ya masuala
mbalimbali yahusuyo Bodi yake mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii Mh.
Profesa Jumanne Maghembe wakati wa mkutano na Menejimenti ya TTB leo.
Kulia kwa Bi Devota ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na
Utalii Bibi Agelina Madata.
Wajumbe wa Menejimenti ya TTB
wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Bw. Ramo
Makani (wa pili kulia katika meza kuu) leo jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………………….
Waziri
wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe (MB) ameitaka Bodi ya Utalii
Tanzania- TTB kuendelea kutumia vyombo vya habari vya Kimataifa kama vile CNN, BBC
n.k kuitangaza Tanzania kama eneo la Utalii duniani sambasamba na kuweka makala
na matangazo ya utalii wetu katika majarida ya Kimataifa yanayoandika habari za
Utalii na usafiri (Travel Magazine) ambayo ndiyo husomwa na watalii wengi duniani.
“Kama kweli tunataka kupata watalii wengi
zaidi pamoja na mambo mengine ni lazima tutumie vyombo vikubwa vya Kimataifa
vinavyofikia watu wengi zaidi duniani” alisema na kuongeza kuwa pamoja na njia
nyingine zinazotumiwa katika kuitangaza Tanzania kimataifa, mbinu hii ya
kutumia vyombo vya habari yaweza kuwa na ufanisi mkubwa zaidi .

Maghembe ameyasema hayo leo alipotembelea Bodi ya Utalii Tanzania na kukutana
na Menejimenti ya TTB kwa lengo la
kujitambulisha na kubadilishana mawazo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Bodi
katika utangazaji utalii ndani na nje ya nchi.

Akizungumzia
kuhusu madeni makubwa yanayoikabili TTB, Mh. Profesa Jumanne Maghembe ameahidi kuwa
Wizara yake itachukua madeni yanayoikabili TTB na hasa yaliliyotokana na
maelekezo ya Wizara ya kama yale yaliyotokana na kuitaka Bodi iingie mikataba
ya kuweka matangazo katika ligi kuu ya Uingereza na klabu za mpira wa mguu na
Sunderland Football Association pia ya nchini Uingereza. Amesema Wizara ni
lazima ilipe madeni hayo ili kulinda taswira ya Bodi ya Utalii kwa wadau na
kuiondolea Bodi mzigo wa kuhangaikia madeni hayo badala yake ijikite zaidi
katika kutangaza utalii.Kuhusu
ukuzaji na uendelezaji wa utalii nchini Profesa Maghembe amebainisha kuwa
pamoja na uwepo wa mashirika mbalimbali ya ndege yanayokuja hapa nchini lakini
kuna haja kubwa Tanzania kuwa na shirika lake imara la ndege ambalo litasaidiasana kukuza utalii nchini kama ilivyo kwa nchi nyingine kama Kenya na Afrka ya
Kusini. Aidha amesema kuna haja pia ya kuboresha na kuendeleza zaidi vivutio vyetu vya utalii na mazao mengine ya
utalii kama vile Utalii wa fukwe na
Utalii wa utamaduni sambasamba na kukamilisha zoezi la uwekaji madaraja
hoteli zetu na kutoa elimu kwa wenye hoteli kuboresha zaidi hoteli zao na
hudiuma watoazo.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na viongozi wengine kutoka Wizarani akiwemo Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Bw. Ramo Makani, Naibu katibu Mkuu Bi Angelina
Madata na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Bw. Zahoro, Waziri Maghembe amesema anataka
kuona idadi ya watalii ikiongezeka kutoka 1,100,000 ya sasa na kufikia Milioni
3,000,000 mwaka 2018. Mapema kabla ya kumkaribisha waziri kuzungumza na Menejimenti, Kaimu Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Bi Devota Mdachi alimwelezea Mh. Waziri mafanikio
kadhaa ambayo Bodi imeyapata ikiwa ni pamoja na kuanzisha onesho la Utalii la Kimataifa
la Swahili Swahili International Tourism Expo (S!TE) linalofanyika kila mwaka
jijini Dar es salaam, kuanzishwa kwa tovuti maalumu (Portal) ya kuitangaza
Tanzania na kulipia huduma nyingine za utalii moja kwa moja , uwekaji wa
matangazo sehemu mbalimbali duniani. Bi Devota alimfahamisha pia Mh. Waziri kuwa TTB imechaguliwa kuwa miongoni mwa
Bodi za Utalii tatu bora barani Afrika ambazo zinashindanishwa kumpata mshindi
wa kwanza na wa pili. “Mh. Waziri, pamoja na matatizo mengi yanayoikabili TTB
lakini tunafurahi kukujulisha kuwa TTB ni miongoni mwa bodi za utalii tatu
zilizoingia katika hatua ya mwisho ya kutafuta mshindi wa Bodi ya Utalii borani
Afrika tukishindana na Bodi za utalii za Afrika ya Kusini na Namibia katika
shindano linaoendeshwa na taasisi ya Travvy ya Marekani” alidokeza Bi Mdachi.

Kaimu Mkurugenzi huyo alidokeza pia kuhusu
changamoto kadhaa zinazoikabili Bodi kubwa zaidi ikiwa ni madeni makubwa ya nje
na ndani, na bajeti ndogo ya utangazaji.

No comments:
Post a Comment