Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni
inayojishughulisha na uandaaji wa Filamu ya Didas Entertainment Bibi.
Khadija Seif (Dida) (akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo
wakiwa katika ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Ally Daud,MAELEZO
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) akimsikiliza kwa makini Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Didas Entertainment Bibi. Khadija Seif
(Dida) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.Kampuni
hiyo inajishughulisha na udhamini wa wasanii nchini.
………………………………………………………………………………………………………..
Na: Frank Shija
Serikali imepongezwa kwa namna inavyotoa ushirikiano na kusaidia wasanii na wadau wa tasnia ya Filamu hapa nchini.
Pongezi hizo zimetolewa na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Didas Entertainment Bibi. Khadija Seif
(Dida) alipotembelea ofisi za Bodi ya Filamu leo jijini Dar es Salaam.
Dida amesema kuwa kama mdau wa
Filamu anaishukuru na kuipongeza Serikali namna ambavyo inathamini na
kutambua mchango wa wadau wa tasnia hiyo hapa nchini.
“ Naishukuru Serikali kwa namna
ambavyo imekuwa ikitoa ushirikiano kwetu sisi wadau wa tasnia ya filamu
hapa nchini” Alisema Dida.
Aidha Dida amesema kuwa kupitia
Kampuni yake ya Didas Entertainment yenye ofisi zake jijini London ipo
katika uaandaaji wa Filamu mbili ambazo ni “Dida” na “Black Belt”
zitakazo tengenezewa hapahapa nchini.
Nakuongeza kuwa filamu hizo
zitakuwa shirikishwa baadhi ya wasnii kutoka Nigeria na zitakapo
kamilika Filamu ya Black Belt inatarajiwa kuzinduliwa katika nchini nne
tofauti ambazo ni Uingereza, Nigeria, Ghana na Tanzania
Kwa upande wake Katibu Mtendaji
wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesma kuwa Serikali itaendelea
kushirikiana na wadau wa tasnia Filamu wandani na njje ya nchi ili
kutanua wigo wa tasnia hiyo kukua kwa kasi.
Fissoo ametoa wito kwa wadau wa Filamu kuja kuwekeza katika tasnia Filamu hapa nchini ili kutanua wigo wa filamu za Kitanzania
Didas Entertaiment imekuwa msaada
mkubwa kwa tasnia za Filamu na Muziki ambapo mpaka sasa imewezesha
takribani wasanii 30 kupata maonyesho nchini Uingereza, na imefanikiwa
kutengeneza Filamu moja ya “Mateso yangu Ughaibuni”ambayo inafanya
vyema katika soko.Kampuni hii imefungua milango kwa wasanii wa Filamu
ili kutanua wigo wa Filamu za Kitanzania.
No comments:
Post a Comment