Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na
baadhi ya wafanyakazi wa TPA eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini
(KOJ) Kurasini jana jiji Dar es salaam. Wa kwanza kulia Mhandisi
anayefanya kazi eneo la KOJ Jabiri Muyones.
Kapteni
Abdulla Mwingamno (kulia) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) baadhi ya vifaa vya kituo cha
kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini jana jiji Dar es
salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongozana na
Mhandisi anayefanya kazi eneo la KOJ Jabiri Muyones alipotembelea TPA
eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini jana jiji Dar
es salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikagua baadhi
vipuri eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini jana
jiji Dar es salaam.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
…………………………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amemuagiza Kaimu Meneja Msaidizi wa
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Nelson Mlali kufanya uhakiki wa
kampuni zinazotoa huduma mbalimbali bandarini ili kuboresha utendaji
kazi na kuepuka mgongano wa maslahi binafsi minongoni wa watumishi wa
bandari.
Profesa Mbarawa alitoa kauli hiyo
baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana jioni(29/03/2016) kwenye ofisi
za Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) eneo la kupakulia mafuta
yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini.
“Mtafanyaje kazi na mtu ambaye ni
mfanyakazi na huku kampuni yake inatoa huduma bandarini, hamuoni
kutakuwa na mgongano wa kimaslahi binafsi,” alihoji Profesa Mbarawa.
Aidha, Prof. Mbarawa amemtaka
Kaimu Meneja Msaidizi Mlali azingatie umiliki wa makampuni kulingana na
taarifa za Wakala wa Usajili wa Biashara na Kampuni nchini (BRELA)
katika zoezi la kuhakiki kampuni hizo.
Akiwa eneo la (KOJ) Kurasini,
Prof. Mbarawa amewataka wafanyakazi wa TPA wabadilike na kufanya kazi
kwa juhudi na maarifa badala ya kufanya kazi kwa mazoea ili kuboresha
kuongeza ufanisi na kuliongezea taifa mapato kwa manufaa ya wananchi
Prof. Mbarawa amewaagiza pia
Mamlaka ya Bandari wanaponunua vipuri na vifaa mbalimbali
vinavyohitajika bandarini hapo wazingatie vipimo sahihi kulingana na
vifaa vinavyohitajika kuendeshea mitambo mbalimbali ili kulipunguzia
taifa gharama zisizohitajika.
Mamlaka ya Bandari nchini ina bandari mbalimbali zilizopo katika ukanda wa bahari ya Hindi na maziwa yaliyopo nchini.
Ukanda wa Bahari ya Hindi una
bandari ya kuu za Dar es salaam, Tanga na Mtwara pamoja na Bandari ndogo
zilizopo Lindi, Kilwa Masoko, Mafia, Bagamoyo, Pangani na Kwale.
Bandari nyingine ziliozo katika
maziwa mbalimbali nchini ni pamoja na Ziwa Victoria lenye bandari ya
Mwanza, Bukoba, Kemondo, Musoma na Nansio, Ziwa Tanganyika likihusisha
bandari ya Kigoma na Kasanga wakati Ziwa Nyasa kuna bandari ya Itungi,
Manda, Liuli na Mbaba Bay.



No comments:
Post a Comment