MGOMO wa kisiasa unaoendelea
Kisiwani Pemba juzi ulichelewesha kwa muda wa saa kadhaa mazishi ya
marehemu Bi Achia Khatib wa Mjini Wingwi Wilaya ya Micheweni , baada
ya msikiti uliokuwa utumike kuswalia mwili wa marehemu kufungwa kwa
kufuli .
Mbali na kitendo cha kufungwa kwa
msikiti huo , pia baadhi ya vifaa vilivyokuwa vitumike katika mazishi
hayo kufichwa ikiwemo kitanda (jeneza) pamoja na mitaimbo ya kuchimbia
kaburi kwani sehemu hiyo ni ya mawe .
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi mmoja wa wanafamilia , Said Omar Said alisema kuwa hali hiyo
ya sintofahamu ni imetokea ikimhusisha mtoto mkubwa wa marehemu
Abdalla Kombo ambaye ni Mwenyekiti wa CCM kijijini hapo .
Alifahamisha kwamba wananchi
waligoma na kusababisha kufungwa kwa msikiti , wakidai kwamba hawako
tayari kushiriki mazishi , hadi pale mtoto wa marehemu (Mwenyekiti wa
CCM) atakapoondoka katika msiba huo .
“Unajua mzee wetu alikuwa ni
mfuasi wa CUF , lakini sasa mtoto wake mkubwa ni mwanaCCM , hivyo
alitaka aondoke ili washiriki mazishi hayo ”alieleza Said Omar Said kwa
maskitiko .
Sheha wa Shehia ya Mjini Wingwi
Shehe Yussuf Hamad aliiambia gazeti hili kwamba , wananchi hao walitaka
pia kuzuia makaburi yasitumike kumzika marehemu , lakini serikali ya
kijiji ililazimika kutumia nguvu kutumika kwa makaburi hayo .
Alisema kwamba visa vingi vya
maajabu vilitokea katika msiba huo , kwani hata sindano ya kushinea
sanda ilichukuliwa na mtoto mdogo wa marehemu Hamad Kombo na kuifichwa
wakati kazi ya ushinaji wa sanda ikiendelea.
Hali hiyo iliwafanya ndugu na
jamaa wa karibu kuomba msaada kutoka vijiji jirani ikiwemo Micheweni na
Majenzi , ambapo wakaazi wa vijiji hivyo ndio waliosaidia kupatikana
sanda na kitanda cha kubebea mwili wa marehemu .
Imamu wa msikiti wa Ijumaa katika
Shehia hiyo Bakar Abdalla alipotafutwa kwa njia ya simu alikana
kuhusika na kitendo cha kufungwa msikiti , na kusema hata taarifa za
kuvunjwa kufuli hajazipata .
Aidha alifahamisha taarifa za
kifo cha bibi huyoa anazo , lakini taarifa za wapi swala ya kumswalia
maiti itafanyika katika msikiti huo hakuwa na taarifa .
“Taarifa ya kifo nilizipata
lakini sehemu ambayo swala itafanyika sikuwa na naelewa , mimi nafahamu
kwamba ulikotokea msiba kuna msikiti mwengine mdogo na ndio uliotumika
kumuswalia maiti ”alieleza.
Kamati ya Ulinzi na Usalama
ikiongozwa na Mwenyekiti wake Abeid Juma Ali ilifika katika eneo la
tukio na baada ya mazungumzo na baadhi ya wazee katika shehia hiyo
yaliyochukua muda wa saa mbili , walilazimika kuvunja kufuli katika
msikiti huo .
Akizungumza na baada ya tukio la
kuvunja kufuli , Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ambaye pia ni Mkuu wa
Wilaya hiyo alilaani kitendo hicho na kuwataka wananchi kushirikiana na
pamoja katika shughuli za kijamii .
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya
alikemea nyumba za ibada kutumika kwa masuala ya siasa na kuahidi
kulitafutie ufumbuzi suala hilo kwa kukutana na mashekhe wote na maimamu
wa misikiti yote Wilayani hapa .
“Hichi kitendo kwa kweli si cha
kiungwana huwezi kumsusia maiti kwa misingi ya kisiasa , nimepanga
kukutana na mashekhe wote wa wilaya tulizungumzie ikiwezekana kuweka
maazimio lengo ni kudumisha upendo “ alieleza.
Mazishi hayo ambayo yalipangwa
kufanyika majira ya saa saba za mchana , yalifanyika saa kumi na moja za
jioni baada ya wanaccm kutoka shehia na vijiji jirani kufika na
kusaidia shughuli za kuustiri mwili wa marehemu .
No comments:
Post a Comment