
Katika chumba namba moja, 
madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakifanya upasuaji wa 
pua kwa mgonjwa LEO kwa kushirikiana na madaktari kutoka Hispania. 
Kutoka kushoto ni Martin Mushi, Pedro na Carlos wakifanya upasuaji kwa 
mgonjwa mwenye matatizo katika mfumo wa pua.
Chumba namba mbili, madaktari wakifanya upasuaji wa masikio kwa mgonjwa mwenye tatizo masikio LEO.
Madaktari wakiendelea na upasuaji wa masikio LEO katika chumba namba mbili.
Madaktari wakifanya maandalizi kabla ya kufanya upasuaji LEO katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
………………………………………………………………………………………..
Neema Mwangomo, PRO MNH
Dar es Salaam, Tanzania. 
Madaktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) 
kwa kushirikiana na timu ya Madaktari wanne kutoka nchini Hispania 
waaendesha zoezi la upasuaji wa masikio , pua pamoja upasuaji wa shingo 
na kichwa (Head and  Neck Surgery).
Akizungumzia kuhusu zoezi hilo 
Daktari Bingwa wa magonjwa ya masikio, Pua na koo Martin Mushi amesema 
katika upasuaji huo madaktari hao wanatumia teknolojia kubwa na ya 
kisasa zaidi ambapo pamoja mambo mengine ujio wao utawawezesha madaktari
 wa Muhimbili  kujifunza zaidi matumizi ya teknolojia mpya ya upasuaji 
(ENDOSCOPY SURGERY).
Akifafanua Daktari Mushi 
amesema awali wagonjwa hao walikuwa wakipelekwa nje ya nchi kwa ajili ya
 upasuaji, lakini kwa sasa wagonjwa wanaohitaji upasuaji wa kawaida 
wanapata huduma hiyo hopa Muhimbili.
Kwa mujibu wa Daktari Mushi, 
 tangu zoezi  hilo lianze  jumatatu ya wiki hii mpaka sasa  wagonjwa 
 16  tayari  wamefanyiwa upasuaji  na kwamba hadi kukamilika kwa zoezi 
hilo wagonjwa  kati ya 25 hadi 30 watakuwa wamefanyiwa upasuaji huo.
“Zoezi hili linaendelea vizuri 
tunashirikiana vema na wataalamu hawa kutoka nchini Hispania, ni fursa 
nzuri kwakweli kwani  tunabadilishana uzoefu, lakini kubwa zaidi sisi 
kujifunza kutoka kwao,” amesema Dk Mushi.
Zoezi la upasuaji kwa 
ushirikiano  na timu ya watalaamu kutoka Hispania limeanza  Aprili 18 , 
2016 na linatarajia kumalizika April 22, 2016.





No comments:
Post a Comment