KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

April 27, 2016

PAPAA WEMBA KAONDOKA NA UTAMU WAKE

Paris, FRANCE: Congolese singer Papa Wemba performs during a concert at the New Morning, 15 February 2006 in Paris. AFP PHOTO PIERRE VERDY (Photo credit should read PIERRE VERDY/AFP/Getty Images)
Makala: Boniphace Ngumije
Ni majonzi tele katika tasnia ya Muziki wa Dansi, Rhumba na Afro Pop Soukous kufuatia kifo cha mfalme wa aina hizo za muziki, Shungu Wembadio Kikumba ‘Papa Wemba’ aliyefariki duniani usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita baada ya kuanguka jukwaani wakati akitumbuiza huko nchini  Ivory Coast huku ugonjwa wa shambulio la moyo.
Papa Wemba aliyezaliwa Juni 14, 1949 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo atabaki kuwa ‘icon’ kwenye aina hizo za muziki huku kwa watu walioanza kumfuatilia mapema watakumbuka alianza kufahamika akiwa katika bendi maarufu nchini mwake iitwayo Zaiko Langa Langa (Nkolo Mboka).
160424104910_papa_wemba_512x288_bbc_nocreditShungu Wembadio Kikumba ‘Papa Wemba’.
Bendi hiyo iliyokuwa na mashabiki wengi kipindi cha nyuma ilikuwa imesheheni wanamuziki wengi  mahiri wakiwemo kina  Nyoka Longo Jossart, Manuaku Pepe Felly, Evoloko Lay Lay, Bimi Ombale, Teddy Sukami, Zamuangana Enock, Mavuela Simeon, Clan Petrole na wengine wengi.
Baada ya kujenga jina lake katika bendi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1969 jijini Kinshasa, Kongo Papa Wemba aliungana na wanamuziki kadhaa wakiwemo Evoloko Lay Lay, Manuela Somo na Bozi Boziana kuanzisha kundi  lililojulikana kama Isifi Lokole na hiyo ilikuwa mwaka 1974.
Lakini baada ya historia ndefu ya ‘hustle’ za kimuziki mwaka 1977, Papa Wemba alianzisha kundi lake mwenyewe liitwalo Viva la Musica ambalo lilimpa umaarufu zaidi duniani huku akifanya matamasha kila kona akilitumia jukwaa kama mkate wake wa kila siku.
Kazi alizofanya
Zipo nyimbo na albamu nyingi alizofanya, miongoni mwake ni pamoja na Pauline alioufanya mwaka 1970 akiwa na Kundi la Zaiko Langalanga. Mwaka 1995 Alicia albamu ya Emotion ikiwa na wimbo mkali wa Show Me The Way uliovuma sana nchini Tanzania kutokana na mpangilio wa sauti yake.
Mwaka 1996 alifanya Wimbo wa Wake-Up 1996 akishirikiana na mkali mwingine Koffi Olomide. Mwaka 2014 aliachia albamu ya Maître D’école-Teacher. Nyingine ni Esclave, Maria Valencia, Lingo Lingo, Madilamba na Mwasi.
Alikuwa muigizaji
Mbali na uimbaji, Papa Wemba pia alikuwa muigizaji. Alishawahi kushiriki katika Filamu ya La Vie Est Belle- (Maisha ni Bora) iliyofanya vizuri sokoni nchini mwake mwaka 1987.
Skendo
Mwaka 2003, nyota huyo aliyezimika ghafla, alidaiwa kuhusika katika mtandao wa kuvusha mamia ya wahamiaji haramu kutoka DRC kwenda Ulaya.
Papa Wemba alivamiwa na polisi nyumbani kwake jijini Paris, Ufaransa na kufungwa jela miezi mitatu na nusu na baadaye kuachiwa baada ya kutokupatikana na hatia.
Mwaka huohuo aliachia Albamu ya Somo Trop ikiwa na wimbo unaozungumzia kile kilichomkuta maishani mwake.
Alikuja Bongo
Mwaka jana Papa Wemba alitua Bongo kwenye Tamasha la Karibu Music Festivals 2015 lililofanyika Novemba 6, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na kuacha historia ya aina yake baada ya kufanya makamuzi makali huku mashabiki waliojitokeza katika tamasha hilo wakiifurahia sauti yake isiyozeeka na umahiri mkubwa aliouonesha.
Koffi Olomide atoa salamu za rambirambi
Baada tu ya taarifa za kifo cha mkali huyu kusambaa Koffi Olomide aliandika ‘coment’ fupi kwenye ukurasa wake wa Twitter uliosomeka “Kwa kheri kaka, Asante’.
Hadi tunaingia mtamboni taarifa juu ya mazishi zilikuwa hazijatolewa na mwili wake ulikuwa bado  uko nchini Ivory Coast. (GPL)



No comments:

Post a Comment