 Mfungaji
 wa CDA Dodoma, Tatu Fungo akiuwahi mpira katika mchezo wao wa netiboli 
wa Kombe la Mei dhidi ya Uchukuzi SC. Uchukuzi walishinda kwa magoli 
23-16.
 Mfungaji
 wa CDA Dodoma, Tatu Fungo akiuwahi mpira katika mchezo wao wa netiboli 
wa Kombe la Mei dhidi ya Uchukuzi SC. Uchukuzi walishinda kwa magoli 
23-16. Mchezaji
 Mwadawa Hamisi wa Uchukuzi SC (GK) akiangalia mwenzake wa kumrushia 
baada ya Tatu Fungo wa CDA kufunga bao katika michuano ya Mei Mosi. 
Uchukuzi walishinda magoli 23-16.
Mchezaji
 Mwadawa Hamisi wa Uchukuzi SC (GK) akiangalia mwenzake wa kumrushia 
baada ya Tatu Fungo wa CDA kufunga bao katika michuano ya Mei Mosi. 
Uchukuzi walishinda magoli 23-16. Mchezaji
 Matalena Mhagama wa Uchukuzi SC (GS) akijiandaa kupokea mpira kutoka 
kwa Tatu Kitula aliyezuiwa na Catherine Ukunguala, katika mchezo wa 
netiboli wa mashindano ya Mei Mosi.
Mchezaji
 Matalena Mhagama wa Uchukuzi SC (GS) akijiandaa kupokea mpira kutoka 
kwa Tatu Kitula aliyezuiwa na Catherine Ukunguala, katika mchezo wa 
netiboli wa mashindano ya Mei Mosi.
……………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TIMU ya netiboli ya Uchukuzi SC jana 
ilianza vyema mchezo wake wa kwanza kwa kuwaicharaza CDA ya Dodoma 
katika mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea mkoani Dodoma.
Uchukuzi SC inayoundwa na wachezaji 
wakongwe, akiwemo mfungaji mahiri wa timu ya Bandari na Taifa, Matalena 
Mhagama waliwapeleka puta wapinzani wao ambapo hadi mapumziko walikuwa 
mbele kwa magoli 11-6.
Katika mchezo huo uliokuwa umetawaliwa na
 rafu za hapa na pale na kulalamikiwa mara kwa mara na wachezaji wa 
Uchukuzi SC, ulimalizika kwa mfungaji Matalena kufunga magoli 16 na Tatu
 Kitula akifunga saba, wakati wapinzani wao Tatu Fungo nma Margeth 
Nicholaus kila mmoja akifunga magoli nane.
Kocha Mkuu wa Uchukuzi SC, Judith Ilunda 
alisema wamepata ushindi huo wa kwanza kutokana na kufanya mazoezi ya 
pamoja ya muda mrefu, pamoja na kwamba wapinzani wao walikuwa ni wazuri 
na wenye uzoefu mkubwa.
“Wengi waliocheza na kikosi change ni 
wakongwe wapo niliocheza nao mimi kwenye mashindano mbalimbali, hivyo 
wameweza kutumia ukongwe wao lakini tuliwazidi mbinu kutokana na timu 
yetu kuundwa na chipukizi wengi,” alisema Ilunda.
Lakini, alilalamikia maamuzi ya waamuzi 
waliocheza mchezo huo kuwa mengi yamepitwa na wakati kutokana na sheria 
kubadilika mara kwa mara.
“Hawa waamuzi wamekuwa wakichezeshakwa 
sheria nyingi za zamani na kusababisha mvutano, hivyo wanatakiwa 
wabadilike kwa kujisomea mara kwa mara ili kuondoa mkanganyiko kwa timu 
zinazocheza,” alisema Ilunda.
Hatahivyo, waamuzi Mariam Makisi na 
Caroline Paulo wote wa Dodoma, kwa nyakati tofauti walisema wamechezesha
 mchezo huo kwa kanuni na sheria za mchezo huo, lakini wameshangazwa na 
malalamiko ya kuwa wamechezesha kwa sheria za zamani.
“Unajua timu za Dar es Salaam siku zote 
zinajifanya kujua sheria zaidi, na wangeweka wazi ni wapi waamuzi 
tulipopindisha sheria,” alisema  Makisi.
Wakatihuohuo, timu ya Tamisemi iliwafunga TPDC kwa magoli 6-1 katika mchezo wa soka uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri.
Wafungaji wa Tamisemi ni Mwigane Yeya 
kafunga magoli mawili, wakati waliofunga moja-moja ni Hamis Shedafa, 
Hamad Majura, Nelson Richard na Phillipo Oden; wakati bao la kufutia 
machozi la TPDC lilifungwa na Shija Dalushi.
Katika mchezo mwingine wa soka, timu ya 
Tanesco ilipata ushindi wa chee baada ya wapinzani wa CWT ya Dodoma 
kushindw kutokea uwanjani.
 


 
No comments:
Post a Comment