Mbunge
 wa Kavuu, Dk Prudenciana Kikwembe (CCM) ameitaka Serikali kueleza ni 
lini itatoa fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo kwa wakati.
Dk
 Kikwembe akiuliza swali la nyongeza bungeni, alisema mara nyingi fedha 
za maendeleo zimekuwa zikipelekwa katika maeneo husika kwa kuchelewa na 
hivyo kuchelewesha miradi mingi.
“Ni
 lini fedha za utekelezaji wa shughuli za maendeleo zitatolewa kwa 
wakati na fedha zinapochelewa na kutolewa mwishoni mwa mwaka wa fedha, 
fedha hizo huwa zinaenda wapi?”Alihoji Dk Kikwembe.
Akijibu
 swali hilo, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
 Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo alikiri kuwa miradi mingi ya maendeleo
 imekuwa ikisuasua kutokana na ukosefu wa fedha.
Hata
 hivyo alisema, kutokana na jitihada zilizopo za kukusanya mapato ya 
Serikali, tayari baadhi ya miradi iliyokwama imeshaanza kutekelezwa na 
anaamini miradi yote iliyokuwa imekwama itatekelezwa kabla ya kumalizika
 kwa mwaka huu wa fedha.
Awali,
 katika swali la msingi Mbunge huyo alitaka kujua ni lini kata ya Mamba,
 Majimoto, Chamaledi na Mwampuli zitapatiwa maji safi na salama .
Akijibu
 swali hilo Jaffo alisema ili kutatua changamoto ya maji katika kata ya 
Mamba, Serikali imetenga Sh milioni 24 katika bajeti ya mwaka 2015/2016 
kwa ajili ya kuchimba kisima kirefu katika kijiji cha Ntaswa ambacho 
hakina maji kati ya vijiji vilivyopo.
Alisema
 vijiji ambavyo havijapata huduma ya maji katika kata ya Majimoto ni 
Kuchimba na Ikulwe ambavyo alisema vimetengewa Sh milioni 48.4 katika 
bajeti ya mwaka 2015/2016 kwa ajili ya kuchimba visima virefu kila 
kijiji.
 



 
No comments:
Post a Comment