KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

April 1, 2016

WAFADHILI WASITISHA UFADHILI KWA BAJETI YA TANZANIA

Rais John Pombe Magufuli
Mataifa 10 ya Magharibi yamesema hayataendelea na ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania.
Baadhi ya nchi hizo ni Sweden na Ireland. Nchi hizo zinaendelea na msimamo huo ikiwa ni siku chache baada ya shirika la utoaji misaada la serikali ya marekani (MCC) kuondoa msaada wake wa awamu ya pili wa dola milioni 472 sawa na Sh.tirilioni moja za ufadhili wa miradi ya maendeleo kwa Tanzania.
Bodi ya MCC ilisema hatua yake ilitokana na mzozo kuhusu uchaguzi wa kisiwa cha Zanzibar na utekelezwaji wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao.
Mataifa yaliyositisha ufadhili wao kwa bajeti ya Tanzania hata hivyo hayajaeleza sababu ya kufanya hivyo.
Ubalozi wa Sweden umethibitisha kwamba taifa hilo limesitisha ufadhili wake kwa bajeti ya Tanzania, lakini ukasisitiza kwamba hatua hiyo haihusiani na yaliyojiri katika uchaguzi wa visiwa vya Zanzibar. BBC

No comments:

Post a Comment