![]() |
| Kamishna Jenerali wa
Magereza Nchini, John Casmir Minja leo tarehe 18 Mei, 2016 saa 8:00
mchana atawavisha vyeo Maafisa wa Jeshi la Magereza wa ngazi mbalimbali
wa Mkoa wa Dar es Salaam waliopandishwa vyeo kwa mujibu wa Sheria.
Kwa Mamlaka aliyopewa
kisheria na Tume ya Polisi na Magereza ya Mwaka 1990, Kamishna Jenerali
wa Jeshi la Magereza atawavisha vyeo hivyo katika Viwanja vya Chuo cha
Taaluma ya Urekebishaji kilichopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Tume ya Polisi na Magereza
katika Kikao chake Namba 5/2015/2016 kilichofanyika tarehe 13 Mei, 2016
chini ya Mwenyekiti wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles
Kitwanga(Mb) imewapandisha vyeo Maafisa 310 wa ngazi mbalimbali kuanzia
tarehe 16 Mei, 2016.
Maafisa hao waliopandishwa vyeo ni Mrakibu Mwandamizi wa Magereza
kuwa Kamishna Msaidizi wa Magereza 45, Mrakibu wa Magereza kuwa Mrakibu
Mwandamizi wa Magereza 37, Mrakibu Msaidizi wa Magereza kuwa Mrakibu wa
Magereza 90 na Mkaguzi Msaidizi wa Magereza kuwa Mkaguzi wa Magereza
138.
Imetolewa na; Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Lucas Mboje, Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM 18 Mei, 2016. |
May 18, 2016
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI KUVISHA VYEO MAAFISA WA JESHI LA MAGEREZA, LEO JIJINI DAR
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment