![]() |
| Na Tiganya Vincent-MAELEZO_Dodoma.
Wizara ya Maliasili na Utalii
imesema kuwa inatarajia kuboresha utalii wa kusini mwa Tanzania kupitia
miradi mbalimbali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo chini ya mradi
wa REGROW unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa gharama za shilingi
bilioni 2.1.
Fedha hizo zinafadhiliwa na Benki ya Dunia sawa na Dola za Kimarekani zisizopungua milioni moja.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini
Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Injinia Ramo Makani
wakati akijibu swali Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini Mhe. Hassan Kaunje
aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kuendeleza utalii wa ukanda wa
kusini.
Alisema kuwa hatua hiyo
inalenga kuwekeza katika miundombinu ya utalii kwa ajili ya kuutangaza
utalii wa Ukanda wa Kusini mwa Tanzania ili uweze kusaidia ukuaji wa
uchumi na ustawi wa Taifa.
Alisema kuwa mpango huo
utajumuisha kuimarisha mafunzo ya utalii na kutenga maeneo maaalum ya
utalii katika fukwe za bahari na maziwa kwa ajili hoteli za kitalii.
Mhe. Makani alisema kuwa
Serikali imepanga kutekeleza mkakati wa kuutangaza maeneo ya utalii
ikiwemo vivutio kihistoria na kiutamaduni kama vile mji wa kihistoria wa
Mikindani, Kilwa Kivinje, Pori la Akiba Lukwika-Lumese na Pori la Akiba
la Seleous.
Aliongeza kuwa ili kukuza
utalii wa fukwe katika eneo hilo , Serikalai imejipanga kutenga maeneo
maalum hususan kwa ajili ya hoteli za kitalii kando ya Bahari ya Hindi
mkoani Mtwara na Lindi.
|
May 18, 2016
MALIASILI NA UTALII KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KUWEKEZA KATIKA UTALII WA KUSINI MWA TANZANIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment