![]() |
| Na Tiganya Vincent_MAELEZO-Dodoma.
Jumla ya shilingi bilioni
224.314 (224,314,313,555.30) zimepokelewa na Serikali toka kwa wafadhili
ili kusaidia kupunguza athari na kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini
Dodoma na Naibu Waziri , Ofisi ya Makamu wa Rais ,Muungano na
Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo
la Wawi Mhe. Ahmed Juma Ngwali aliyetaka kujua serikali imeokea kiasi
gani toka kwa wafadhili kusaidia kupunguza athari na mabadiliko ya
tabianchi tangu 2010 hadi 2015.
Alisema kuwa kati ya fedha hizo
shilingi bilioni 7,017(7,017,510,977.40) na shilingi 217.296
(217,296,802,577.90 zilipokelewa moja kwa moja kutoka kwa wadau wengine.
Mhe. Mpina alisema kuwa fedha
hizo zilipatikana baada ya kuandaa miradi kwa kuzingatia vigezo na
viapaumbele vya vyanzo vya fedha husika.
Alisema kuwa kati ya fedha hizo
shilingi bilioni 17.2 zilipelekwa Zanzibar kwa ajili miradi ya ujenzi
kutwa katika baadhi ya maeneo ya bahari ambayo yameanza kuathirika na
upandaji wa mikoko ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Mhe. Mpina alisema kuwa fedha
hizo zimepokelewa kutoka Mifuko iliyo chini ya Mkataba wa Mabadiliko ta
Tabianchi na ushirikiano na nchi wafadhili.
|
May 18, 2016
TANZANIA YAPOKEA BILIONI 224 KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment