Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Daudi Ntibenda (kushoto) akizungumza na waandishi wa
habari baada ya kupokea msaada wa madawati 100 kutoka Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). Katikati ni Afisa Mwandamizi wa
Itifaki na Uhusianoi wa AICC, Catherine Kilinda. ………………………………………………………………………
Kituo cha Mikutano cha KimataifaArusha (AICC)kimemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Daudi Ntibenda madawati 100 yenye thamani shilingi milioni nane ili kupunguza tatizo la upungufu wa madawati katika mkoa huo.
Akipokea
madawati hayo jijini Arusha jana, Ntibenda amesema kwamba msaada huo ni
sehemu ya juhudi za serikali mkoani Arusha kuwashirikisha wadau wa
maendeleo ili kuhakikisha shule
zote za mkoa huo zinakuwa na madawati ya kutosha.
“Napenda niishukuru sana AICC kupitia kwa Mkurugenzi Mwendeshaji Elishilia Kaaya kwa kuitikia
vema wito wa serikali ya mkoa wa kuomba wadau wasaidie kuondoa tatizo la upungufu wa madawati katika mkoa wetu”, alisema Mkuu wa Mkoa.
Alitoa wito kwa wadau mbalimbali mkoani Arusha wakiwemo wafanyakazi
wa ofisi ya Mkoa wa Arusha nao kujitokeza ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha kila mwanafunzi ana kaa katika dawati.
Akizungumza
baada ya kukabidhi madawati hayo, Afisa Mwandamizi waItifakina Uhusiano
wa AICC, Catherine Kilinda amesema kwamba AICC kama shirika la umma
linawajibu wakuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya
elimu hapa nchini.
“Sisi kama shirika la umma linalojiendesha kibiashara tunaona fahari kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzaia wa kuhakikisha watoto wetu wa shule hawakai chini na ndio maana leo hii tumekabidhi msaada huu ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais katika kuinua sekta ya elimu”, alieleza Catherine.
AICC ambayo inajihusisha na kutoa huduma za Mikutano, upangishaji w ofisi na nyumba pamoja
na kutoa huduma za afya, imekuwa ikitumia sehemu ya faida katika kusaidia jamii hasa katika sekta ya elimu. |
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Ntibenda (kushoto) akipokea madawati kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa Itifaki na Uhusiano wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Catherine Kilinda. AICC imechangia madawati 100 kuunga mkono juhudi za serikali kuhakikisha shule zinakuwa na madati ya kutosha. |
No comments:
Post a Comment