………………………………………………………………………………………………..
Na Felix Mwagara, MOHA
KATIBU
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira amesema fedha za kuwalipa watumishi 597 waliositishiwa
mikataba yao katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) zipo na
watalipwa hivi karibuni.
Rwegasira
alisema kiasi cha shilingi bilioni 2.3 zimetengwa kwa ajili ya malipo
ya Watumishi hao waliachishwa kazi Machi 7, 2016 ambapo wanaidai Mamlaka
mishahara ya miezi mitatu nyuma, malimbikizo ya fedha katika Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii na makato ya fedha za Bima ya Afya.
Akuzungumza
na watumishi wa Makao Makuu ya NIDA pamoja na Maafisa Wasajili wa
Vitambulisho vya Taifa, jijini Dar es Salaam jana, Rwegasira aliwataka
watumishi hao waliositishiwa mikataba yao, wasipotoshwe na mtu yeyote
kuhusu kutokulipwa haki zao kwani wapo katika hatua ya mwisho ya
kukamilisha taratibu ndogo ndogo kabla ya kuanza kuwalipa.
“Naomba
muwaambie waondoe wasiwasi wowote, waache maneno, watulie kwani
Serikali ipo makini na fedha tunazo na tutaanza kuwalipa mara tumalizapo
taratibu ndogo ndogo zilizobaki.” Alisema Rwegasira.
Aidha,
Rwegasira aliwataka watumishi wa Mamlaka hiyo kufanya kazi kwa bidii na
kuhakikisha ifikapo Desemba 31 mwaka huu Watanzania Milioni 23
wanatakiwa watambuliwe na kupata namba kabla ya kuanza kupewa
Vitambulisho vya Taifa.
Hata
hivyo, watumishi hao walimuakikishia Katibu Mkuu huyo, kuwa kazi hiyo ya
utambuzi itakamilika kama ilivyopangwa na itafanyika kwa umakini
mkubwa kama inavyotarajiwa.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modestus Kipilimba alimshukuru
Katibu Mkuu huyo kwa kuwatembelea na kuwatia hamasa katika kukamilisha
kazi pamoja na kufikisha lengo lao la kukamilisha utambuzi ifikapo
mwishoni mwa mwaka huu.
“Tunakuahidi
Katibu Mkuu kuwa tutatimiza lengo letu na tunakuakikishia tutafanya
kazi kadiri ya uwezo wetu tukiongozwa na kauli mbiu ya ‘hapa kazi tu’,
alisema Dk. Kipilimba
Katibu
Mkuu Rwegasira alifanya ziara hiyo kwa lengo la kujifunza zaidi
shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka, hata hivyo alipata muda wa
kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya
kiutendaji
No comments:
Post a Comment