![]() |
| Kwa
mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya, polisi wanasema hakuna
kilichoibiwa kutoka kwenye gari lake. Simu zake mbili na pesa
vilipatikana ndani ya gari.
Bw Juma alikuwa mwanakandarasi ambaye pia alihusika katika sekta ya uchimbaji madini.
Alikuwa mkurugenzi katika kampuni ya Erad
iliyoshtaki Bodi ya Taifa la Nafaka na Mazao kuhusu kandarasi. Alitaka
alipwe jumla ya Sh500m na bodi hiyo.
Agosti mwaka jana, alimshtaki
Gavana wa jiji la Nairobi Dkt Evans Kidero akitaka akaunti zake za
benki zifungiwe kwa tuhuma kwamba gavana huyo alihusika katika ufujaji
pesa kampuni ya sukari ya Mumias Sugar.
Bw Juma pia alimshtaki
waziri wa madini Najib Balala mwaka jana baada ya leseni ya kampuni yake
ya madini ya Cortec Mining kupokonywa leseni.
Miaka 10 iliyopita,
kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, Bw Juma pia alimshtaki bintiye
rais wa zamani Daniel arap Moi kuhusiana na shamba la ekari 250.
Aidha, aliwasilisha kesi mbili dhidi ya Naibu Rais William Ruto.
|
![]() |
| Gari la Juma lilimiminiwa risasi(Piha na Habari kwa hisani ya BBC) |
Amekuwa akikosoa sana serikali ya Rais Uhuru
Kenyatta na ni mmoja wa waliokuwa wakiishinikiza sana kuhusiana na
sakata ya Eurobond.





No comments:
Post a Comment