KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

May 11, 2016

MKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM AIBUKA KIDEDEA KAMPENI YA AKAUNTI YA MALENGO YA NBC

Gari jipya aina ya Toyota Prado lenye thamani ya shs milioni 167 atakalokabidhiwa mshindi wa kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC, Erastus Vincent Mtui kama linavyoonekana. 
Meneja Masoko wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Alina Maria Kimaryo (wa pili kushoto), akizungumza wakati wa droo kubwa ya kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC jijini Dar es Salaam leo ambapo mkazi wa jiji hilo, Erastus Vincent Mtui (hayupo pichani), alijishindia gari jipya aina ya Toyota Prado lenye thamani ya shs milioni 167. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Malipo ya Mishahara, Amos Lyimo, Meneja kampeni, Mtenya Cheya, Meneja Uwekezaji na Wateja Wakubwa wote wa NBC,  Dorothea Mabonye na Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Mrisho Millao.
 Meneja Kampeni ya Benki ya NBC, Mtenya Cheya (wa pili kushoto), akipiga simu kwa mshindi wa  kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC jijini Dar es Salaam leo ambapo mkazi wa jiji hilo, Erastus Vincent Mtui alijishindia gari jipya aina ya Toyota Prado lenye thamani ya shs milioni 167. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo, Meneja Uwekezaji na Wateja Wakubwa, Dorothea Mabonye na Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Mrisho Millao.
: Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kulia), akizungumza katika hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment