![]() |
UTEUZI WA WENYEVITI NA WAJUMBE WA
BODI YA WAKURUGENZI WA SHIRIKA LA MAKUMBUSHO YA TAIFA, TAASISI YA
UTAFITI WA MISITU TANZANIA (TAFORI) NA BODI YA UTALII TANZANIA (TTB).
……………………………………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi
ya Wakurugenzi wa Shirika la Makumbusho ya Taifa, Bodi ya Taasisi ya
Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Katika uteuzi huo Mhe. Rais
amemteua Bi. Anna Abdallah (Mbunge Mstaafu) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Shirika la Makumbusho ya Taifa, Dkt. Felician Kilahama (Mbobezi katika
fani ya Misitu) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu
Tanzania (TAFORI) na Jaji Mstaafu Thomas Mihayo kuwa Mwenyekiti wa Bodi
ya Utalii Tanzania (TTB).
Kufuatia uteuzi huo wa Mhe. Rais,
Waziri wa Maliasili na Utalii kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya
Shirika la Makumbusho ya Taifa Sura ya 281 kifungu cha 4(2) kikisomwa
pamoja na Jedwali aya ya (1a) amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi
hiyo;
Aidha, kwa mamlaka aliyonayo
chini ya Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) Sura
ya 277 kifungu cha 6(2) kikisomwa pamoja na Jedwali la 2 (1)(a), Mhe.
Waziri amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa taasisi
hiyo;
Pia, kwa mamlaka aliyonayo chini
ya Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) Sura ya 364
kifungu cha 3(2) kikisomwa pamoja na Jedwali 1(2), Mhe. Waziri amewateua
wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa taasisi hiyo;
Uteuzi wa Wenyeviti na Wajumbe hao ni wa muda wa miaka mitatu kuanzia tarehe 24/04/2016 hadi tarehe 23/04/2019.
IMETOLEWA NA:
Angelina E.A. Madete
KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
10 Mei, 2016
|
May 11, 2016
RAIS DK. MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WENYEVITI WA BODI ZA TAFORI NA TTB
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment