Kwa mara nyingine tena Tanzania
inashiriki katika onesho la kimataifa la Utalii la INDABA yanayofanyika
huko Afrika Kusini maonesho hayo yalianza jana tarehe 7 Mei na
yanatarajiwa kumalizika tarehe 9 Mei, 2016. jijini Durdan, Bodi ya
Utalii (TTB) ndio waratibu wa onesho kwa upande wa Tanzania. Katika
onesho hili TTB inashirki pamoja na taasisi za TANAPA na Mamlaka na
Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na makampuni mbalimbali binafsi Zaidi ya 30
ya sekta ya Utalii .
Katika siku yake ya kwanza Banda
la Tanzania limetembelewa na wadau wengi wakiwemo watalii, waandishi wa
habari za utalii, mawakala wa Utalii nk. Miongoni mwa watu mashuhuri
waliotembelea Banda la Tanzania ni Mwandishi maarufu na mtangazaji wa
Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard
Quest ambaye alifurahishwa na vivutio vua utalii nchini Tanzania mara
baada ya kupata maelezo kutoka kwa Maofisa wa Bodi ya Utalii Tanzania
TTB.
![]() |
| Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bwa Philip Sebastian akimuonyesha jambo Mwandishi maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard Quest wakati alipotembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya Utalii Indaba jijini Durban nchini Afrika Kusini.. |
![]() |
| Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bwa Philip Sebastian akimpa maelezo kuhusu vivutio vya utalii nchini Tanzania Mwandishi maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard Quest wakati alipotembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya Utalii Indaba jijini Durban nchini Afrika Kusini Katikati ni Bi Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB. |




No comments:
Post a Comment