Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano katika sekta ya
Mawasiliano Profesa Faustine Kamuzora akizungumza katika uzinduzi wa
Safari za ndege za shirika la ndege la nchini Mauritius jijini Dar es
Salaam leo. shirika hilo limezindua safari za ndege za kutoka nchini Mauritius kwenda jijini Dar es Salaam na kutoka jijini Dar es Salaam kwenda nchini Mauritius ndege hizo zitaanza safari zake kesho.
Mwenyekiti wa shirika la ndege la nchini Mauritius, Dr. Arjoon Suddhoo akizunumza katika uzinduzi wa safari za shirika la ndege la nchini Mauritius
jijini Dar es Salaam leoikiwa na lengo la kuunganisha ushirikiano kati
ya nchi za bara la Afrika hasa Tanzania na Nchi ya Mauritius.Safari hizo ni za kutoka nchini Mauritius kuja Dar es Salaam na Dar es Salaam kwenda nchini Mauritius.
Makamu mkuu wa rais wa shirika la ndege la nchini Mauritius,
Dornald Payen(katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam leo kabla ya kuzindua safari za ndege za shirika la ndee la
nchini Mauritius, kushoto ni Mwenyekiti wa shirika la ndege la nchini Mauritius, Dr. Arjoon Suddhoo na kulia ni Mrs Kan oye Long akiwa katika mkutano wa waandishi wa habari



No comments:
Post a Comment