Mwenyekiti
wa Gidani Group na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Michezo ya
kubahatisha katika kanda ya Afrika ya Kusini Profesa Bongani Aug Khumalo
akielezea jinsi michezo ya Bahati Nasibu itakavyoendeshwa kwa wananchi
waliofika kwenye Banda la Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ambapo
kampuni hiyo ilishiriki
Mkurugenzi
wa Bodi inayosimamia michezo ya Kubahatisha nchini,Bw, Abbas Tarimba
akiwa na Mwenyekiti wa Gidani Group ,Profesa Bongani Aug Khumalo
……………………………………………………………………………………….
*Mshindi kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 100
Mchezo mkubwa wa kubahatisha
nchini wa Bahati Nasibu ya Taifa utaanza kuchezwa nchini mwezi huu na
tiketi za kushiriki zitaanza kuuzwa katika mikoa yote kuanzia Mei 21
mwezi huu ambapo droo ya kwanza itafanyika Mei 28 ambapo mshindi wa
zawadi kubwa atakuwa milionea kwa kijishindia kitita cha shilingi
milioni 100.
Mchezo huu kwa sasa utaendeshwa
na kampuni ya kimataifa ya michezo ya Bahati Nasibu ya Gidani
International ambayo kupitia kampuni yake tanzu ya Murhandizwa Limited
mwaka jana ilipata leseni ya kuendesha michezo ya bahati nasibu ya Taifa
nchini na kwa muda wote imekuwa ikijenga mazingira ya kuendesha michezo
hii kisasa kutokana na uzoefu wake mkubwa wa kuiendesha katika nchi
mbalimbali.
Bahati Nasibu ya Taifa
itachezesha michezo mikubwa itakayowezesha washiriki kushinda zawadi
kubwa katika mwaka wake wa kwanza wa kuendesha shughuli zake hapa nchini
sambamba na kuweka rekodi barani Afrika na sehemu nyinginezo duniani.
“Katika kusherehekea kuanza kwa
bahati nasibu hii hapa nchini katika michezo ya 6 ya mwanzoni itazalisha
mamilionea kwa kuwa washindi wa droo kubwa watanyakua zaidi ya milioni
1000.Tunategemea maisha ya watu wengi yatabadilika kuwa bora kupitia
bahati nasibu huu pia usambazaji wa tiketi utafanyika kwa utaalamu
mkubwa”.Alisema Profesa Bongani Aug Khumalo, Mwenyekiti wa Gidani Group
na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Michezo ya kubahatisha katika kanda
ya Afrika ya Kusini.
Tiketi za kushiriki bahati
nasibu hii itauzwa shilingi 500 kila moja na zitapatikana nchi nzima
kupitia mtandao wa mawakala wa kampuni pia zitauzwa kwa njia ya
mtandao.Maelezo zaidi ya kushiriki yatatolewa kupitia vyombo vya habari
wakati wa kuuza tiketi ukifika.
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya www.nationallottery .co.tz kuanzia Mei 9,pia taarifa na matangazo juu ya mchezo huu yatapatikana kwenye vyombo vya habari.


No comments:
Post a Comment