![]() |
| Mwenyekiti wa kampuni ya Gidani ambayo ni kampuni mama ya Murhandziwa Limited,Profesa Bongani Aug Khumalo akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na kuanzishwa na mchezo wa Bahati Nasibu ya Taifa itakayoendeshwa na kampuni hiyo nchini katika hoteli ya SeaCliff jijini Dar es Salaam |
![]() |
| kurugenzi Mkuu wa Bodi ya Taifa
ya Michezo ya Kubahatisha nchini,Abbas Tarimba (kulia) na wadau wengine
wa michezo ya kubahatisha wakisikiliza maelezo ya Professa Khumalo
…………………………………………………………………………………………………….
-Mshindi wa zawadi kubwa kunyakua kitita cha milioni 100
Bodi ya michezo ya Kubahatisha nchini (GBT) na kampuni ya Murhandziwa Limited,
ambayo imepewa leseni ya kuendesha Bahati Naibu ya Taifa leo imetangaza
kuwa maandalizi ya kuanza michezo ya Bahati Nasibu ya Taifa
yamekamilika na tiketi zitaanza kuuzwa nchini katika mikoa yote kuanzia
Mei 21 muda wa saa 12 asubuhi.
Mwenyekiti wa kampuni ya Gidani
ambayo ni kampuni mama ya Murhandziwa Limited,Profesa Bongani Aug
Khumalo, amesema wakati umefika kwa wachezaji wa michezo ya kubahatisha
nchini ambapo wataweza kushiriki katika michezo hii katika mazingira ya
uendeshaji wa kitaalamu na weledi mkubwa ambao utawanufaisha wananchi
watakaobahatika kujishindia zawadi na kubadilisha maisha yao.
Alisema tiketi za kushiriki
bahati nasibu zitauzwa kwa shlingi 500 na zitapatikana kwa mawakala
waliosambaa nchini kote na kwa njia ya mtandao na washiriki wa mchezo wa
bahati nasibu ya taifa wanatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 18 na
kuendelea. “Droo ya kwanza kubwa ya mchezo huu itafanyika Mei 28
mwaka huu na droo nyingine zitakuwa zikifanyika kila siku ya Jumatano na
Jumamosi.”Aliongeza Profesa Khumalo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi
ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) Abbas Tarimba amesema kuwa
ushiriki katika michezo ya Bahati Nasibu ya Taifa unachangia jitihada
za serikali za kuwainua wananchi wake kiuchumi na ndio maana kuna
michezo hii na inaruhusiwa kuendeshwa nchini.
Ujio wa kampuni hii ya
Murhandziwa Limited kumeelezwa na Professa Khumalo kuwa mbali na
kuwanufaiha washindi binafsi pia utatoa ajira Zaidi ya 1,000 nchini za
moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja na kudai kuwa kwa sasa tayari
wameajiri wafanyakazi 40 na idadi itaongezeka hadi 120 ambapo pia
kutakuwepo na idadi ubwa ya mawakala wa kuuza tiketi nchini kote.
Pia imeelezwa kuwa kampuni
itabadilisha sura ya mchezo huu kwa na viwango vya kimataifa kutokana na
uzoefu wake na ubunifu pia wafanyakazi wake watapatiwa mafunzo ya
uendeshaji michezo hii kwa viwango vya kimataifa.
Kuhusu kukuza uchumi wa nchi
imeelezwa kuwa Murhandizwa itafanya biashara na watanzania zaidi ya 200
ambao wataiouzia bidhaa mbalimbali na mara uendeshaji wa michezo ukianza
matarajio ya kampuni ni kuchangia dola za kimarekani zipatazo 40
milioni katika uchumi wa taifa.
Pia uendeshaji wa michezo hii umeelezwa kuwa utanufaisha watanzania wanaoendesha biashara mbalimbali watakaokuwa mawakala wake.
Imeelezwa kuwa taratibu za
uendeshaji michezo ya Bahati nasibu ya taifa itafuata kanuni na taratibu
zote za nchi chini ya usimamiz wa Bodi ya Taifa ya Michezo ya
Kubahatisha ambapo Mkurugenzi wake Mtendaji wake Abbas Tarimba alisema
kuwa serikali itahakikisha kanuni na taratibu za kuendesha mchezo huu
zinazingatiwa na kuwataka wananchi kujitokeza kushiriki na kusisitiza
kuwa ushiriki wao utawawezesha wenye bahati kujishindia zawadi kila wiki
na kubadilisha maisha yao wakati huo huo kuchangia mapato ya serikali
kwa njia ya kodi.
Maelezo zaidi ya mchezo yanapatikana katika tovuti ya www.bahatinasibuyataifa.co.tz na habari na matangazo kuhusiana na mchezo yatakuwa yanatolewa kwenye vyombo vya habari nchini.
|




No comments:
Post a Comment