![]() |
| Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Chama cha Ushirika (NANYUM)
wilayani Lindi kitatakiwa kulipa deni la sh. milioni 433 kwa wakulima wa
korosho wilayani humo baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa tukio la
wizi wa fedha hizo lililodaiwa kufanyika Januari, mwaka huu.
Katika taarifa iliyotolewa leo
(Mei 12,2016) na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi inasema kutokana na
tukio lililotokea mnamo Januari 7, mwaka huu majira ya saa 12:30 za
jioni huko kijiji cha Nambahu majambazi wapatao watatu wakiwa na bunduki
huku wakitumia usafiri wa pikipiki walivamia Ofisi ya NANYUM na kupora
pesa taslimu sh. milioni 433.
Taarifa hiyo iliendelea kusema
kuwa siku ya tukio hilo, kiasi cha fedha hizo zilichukuliwa kutoka Benki
ya NMB ya Lindi Mjini zikisindikizwa na polisi hadi kijijini Nambahu
wakiwa na viongozi wa chama hicho Bw. Mohamedi Chilumba na Bw.Hassani
Mundedu na fedha hizo zilikabidhiwa na kupokelewa na chama kupitia
vitabu vya mahesabu.
“Baada ya kupata taarifa ya tukio
kutoka kituo cha polisi Tandahimba, polisi walikwenda kijiji hapo
majira ya saa 4:30 usiku na kuchukua maelezo ya viongozi tisa wa NANYUM
juu ya tukio hilo ambapo walitaka kupewa taarifa kama kulisalia kiasi
chochote cha fedha baada ya tukio.Lakini viongozi hao wote walikana
kwamba hakuna hata kiasi kilichobakia” ilieleza taarifa hiyo.
Aidha taarifa hiyo ilifafanua
kwamba katika uchunguzi wa polisi ulibaini kati ya sh. milioni 443
zilizokabidhiwa kwenye chama hicho kutoka benki ya NMB tawi la Lindi
hazikuibiwa zote. Hivyo baada ya wajumbe wa bodi hiyo kuhojiwa na polisi
jumla ya sh. milioni 32 zilipatikana.
Hadi sasa baadhi ya wajumbe hao wanashikiliwa na polisi ili kubaini upotevu wa fedha hizo.
Taarifa hiyo ilieleza kwamba kama
itathibitika kisheria kwamba viongozi wa chama hicho wamehusika katika
tukio hilo na kupatikana na hatia ya wizi watalazimika kulipa fedha hizo
na Serikali itaendelea kufuatilia matukio kama hayo na kuhakikisha
kwamba wakulima wanapata haki zao.
|
May 13, 2016
CHAMA CHA USHIRIKA NANYUM LINDI CHADAIWA MILIONI 433 NA WAKULIMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment