![]() |
Mgombea mkuu wa chama cha Republican
Donald Trump ameshutumu Uchina na kusema imekuwa “ikiibaka” Marekani
kupitia sera zake za kibiashara.
Ameambia watu waliohudhuria
mkutano wa kisiasa Indiana kwamba Uchina imekuwa ikitekeleza “wizi
mkubwa zaidi kuwani kutekelezwa katika historia ya dunia.”Bw Trump, mfanyabiashara tajiri kutoka New York, amekuwa akiituhumu Uchina kwa kuchezea sarafu yake ili kuwa na ushindani wa kibiashara duniani inapouza bidhaa nje ya nchi. Hilo, amesema, limeathiri sana wafanyabiashara na wafanyakazi wa Marekani. “Hatuwezi kuruhusu Uchina iendelee kuibaka nchi yetu, na hilo ndilo tunafanya (kwa wakati huu),” alisema mkutanoni Jumapili. "Tutabadilisha mambo, na tuna uwezo, msisahau. Tuna nguvu sana dhidi ya Uchina.” Katika manifesto yake ya kampeni, Bw Trump ameahidi kufanikisha mkataba bora wa kibiashara baina ya Uchina na Marekani ambao utawezesha “wafanyabiashara na wafanyakazi kutoka Marekani kuweza kushindana”.BBC |
May 2, 2016
TRUMP NAYE, ADAI ETI CHINA 'INAIBAKA' MAREKANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment