KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

May 1, 2016

TUNACHUKUA UBINGWA KAMA SINEMA YA KIMAREKANI, AJIGAMBA RANIERI KOCHA WA LEICESTER CITY

Image result for leicester city
Kocha wa Leicester Claudio Ranieri anataka 'staili ya sinema' ambayo itawaiwezesha timu yake maarufu kama 'mbweha' kunyakua ubingwa ugenini uwanja wa Old Trafford baadaye leo.

Ushindi huo wa ugenini utaiwezesha Leicester City kunyakua ubingwa ugenini huku wakiwa wamewaacha wanaowafuatia kileleni Tottenham kwa pointi saba na bado Leicester wakiwa na michezo miwili kibindoni.
Image result for leicester city

Hata kama hawatashinda leo , bado wanahitaji pointi tatu katika mechi tatu walizobakiza kutawazwa mabingwa 

"Huwezi amini, hii ni historia, na tunafahamu ," anasema Ranieri raia wa Italia.

"Ni vizuri kumalizia stori kama sinema . Fainali huwa ni safi na mwisho mzuri.

Ranieri alijiunga na Leicester Juni mwaka jana
Msimu uliopita Leicester ilinusurika kushuka daraja, sasa hivi imeandika historia kwa mafanikio waliyoyapata.

1 comment: