KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

May 1, 2016

WADAU WATAKIWA KUENDELEZA MICHEZO

WAM3
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akiwapungia mkono washiriki wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20 alipokuwa mgeni rasmi wakati wa ufungaji wa mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam.Kulia ni Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Riadha Afrika Mashariki Mhandisi Sadick Ibrahim na kushoto ni Makamu wa Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) William Kallaghe.
WAM4Naibu Waziriwa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akisalimiana na Makamu wa Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) William Kallaghe jana jijini Dar es Salaam wakati wa ufungaji wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20.Katikati ni Katibu wa Naibu Waziri Bibi. Anna Nkinda.
WAM5Makamu wa Raisi wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. William Kallaghe akisoma taarifa fupi juu ya mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20 mbele ya Naibu Waziriwa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura(kulia mwenye miwani) jana jijini Dar es Salaam.
WAM6Baadhi ya washiriki wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20 kutoka nchi mbalimbali wakipita mbele ya Naibu Waziriwa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura(hayupo pichani) alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufungaji wa mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam.
WAM8Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (wapili kushoto) akiimba wimbo wa Taifa la Tanzania wakati hafla ya ufungaji wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20  jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Makamu wa Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) William Kallaghe,Raisi wa Shirikisho la Mchezo wa Riadha  Afrika Mashariki Mhandisi Sadick Ibrahim na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo upande wa Miundombinu Alex Nkenyenge.
WAM9Washiriki wa mashindano ya Riadha Afrika ya Mashariki kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20 kutoka nchi mbalimbali wakiimba wimbo wa Taifa la Tanzania wakati wa  hafla ya ufungaji wa mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment