![]() |
| Umoja wa wafanyabiashara
barani Afrika umewataka wafanyabiasha barani humu kuungana na kupaaza
sauti zao ilikuweka mazingira bora ya kufanyabiashara zao kwenye nchi za
bara hili.
Wakizungumza kwenye
mkutano wao wa siku mmoja uliofanyika jijini hapa wamesema mazingira ya
ufanyajibiashara kwenye nchi za bara hili umekuwa na utofauti hali
inayowawia vigumu kutoa biashara sehemu moja kwenda nyingine.
Akizungumza kwenye
mkutano huo mwenyekiti wa umoja huo Peter otafire ambaye pia ni waziri
wa afya wa Uganda amesema kuwa mazingira hayo yamekuwa yakisababisha
ukuaji wa rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.
Alisema kuwa kumekuwa na
muingiliano wa asili kwenye nchi zetu katika mipaka kwa watu
kufanyabiashara toka zama mpaka walipotugawa wakoloni nasi hadi sasa
viongozi wa serikali zetu hawajaweka mazingira bora yaliokuwepo toka
zama hizo.
Alisema kuwa kumekuwepo
na wajasiriamali wadogo ambao mpaka Leo wameshindwa kunyanyuka
kibiashara sababu ya urasimu usio walazima na kuzitaka serikali za bara
hili kuheshimu ripoti ya utafiti wa raisi mstaafu Thabo Mbeki.
”Nadhani imefika wakati
kwetu kubadilika kama tunataka maendeleo ya kiuchumi kwa watu wetu na
kuwepo mazingira bora ya uganyaji biashara kwa sisi wenyewe kwenye bara
hili”alisisitiza brigedia jenerali Otafire.
Nae mfanyabiashara
kutoka nchini Kenya Mahmoud Othao alisema kuwa kitu Kidogo au rushwa
imekuwa chachu ya kutofikiwa malengo kwa wafanyabiasha kwenye mataifa
YETU barani hapa hali inayowafanya kushindwa kufikiwa kwa malengo
tarajiwa.
Alisema kuwa sehemu
kubwa ya wafanyabiashara wamekuwa wabinafsi kuwasaidia wenzao
wajasiriamali kuinuka hali inayositisha ukuaji wa kiuchumi na
kutosaidiana huko kunapelekea kutokuwepo na mazingira mazuri ya mipango
endelevu na urasimu kwa watunga Sera kuegamia wachache.
Mkutano huo uliokuwa
ukijadili ujasiriamali na mikakati ya kuukuza ilikuweza kuleta matokeo
chanya kwa wajasiriamali barani Afrika utakaopelekea kuleta maendeleo ya
kiuchumi
|
May 13, 2016
WAFANYABIASHARA BARANI AFRIKA WATAKIWA KUUNGANISHA NGUVU KUPAZA SAUTI ZAO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment