NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
MFUKO
wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO)
wameanza kutua mafunzo kwa madaktari nchi nzima kuhusu namna ya kubaini na
kushughulikia wahanga wa ajali na magonjwa yanatosababishwa na kazi. Jumla ya
madaktari 380 wa hospitali za rufaa mikoani na wilayani watafaidika na mafunzo
hayo.
Mafunzo yatatolewa kwa siku tano katika vituo vikubwa vinne ikiwemo Dar es salaam,
Arusha, Mwanza na Mbeya. Wataalamu
kutoka ILO waliobobea katika ajali na magonjwa yanayotokana na kazi Dr. Jacques
Pelletier na Dr. Sylvie Thibaudeau ndio watakaoendesha mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba amesema kwamba mafunzo
haya ni hatua muhimu sana kwa Mfuko kwani Mfuko unaanza rasmi ulipaji wa mafao
tarehe 01 Julai 2016 kwa Wafanyakazi wote watakaopata ajali au magonjwa
kutokana na kazi. Miongoni mwa mafao yataayotolewa ni Huduma ya matibabu, Fidia
kwa ulemavu wa muda, Fidia kwa ulemavu wa kudumu, Ukarabati na ushauri nasaha,
Malipo kwa anayemhudumia mgonjwa, gharama za mazishi endapo mfanyakazi
atafariki na fidia kwa wategemezi endapo mfanyakazi pia atafariki.
Bw. Masha Mshomba akifafanua dhumuni kubwa la kufanya haya mafunzo alisema, “Kazi
kubwa ya madaktari hawa itakuwa ni kufanya tathimini ya magonjwa yanayotoka na
kazi na kutupa ushauri wa kuendelea na malipo kama wahusika watakuwa wamepata
ajali au kuugua na wakapata ulemavu”
|
No comments:
Post a Comment