KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 29, 2016

TIMU YA BUNGE YAHAMASISHA WADAU KUCHANGIA MADAWATI.

aks6
Mwenyekiti waTimu ya Bunge (Bunge Sports Club) Mhe. William Ngeleja akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu ya Simba na wapenzi wa timu ya Yanga itakayofanyika mwezi Agosti 2016 kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua tatizo la madawati hapa nchini kwa kuhamasisha wadau kuchangia madawati yatakayo gawanywa katika Halmashauri zote nchini.
…………………………………………………………………………………………………………..
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameandaa mechi maalum kwa ajili ya kuchangia madawati shule za msingi na sekondari, ili kuunga mkono Serikali ya awamu ya Tano kutatua kero ya upungufu wa madawati Nchini.
Mwenyekiti wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club) Mhe. William Ngeleja ameyasema hayo leo Mjini Dodoma katika mkutano na waandishi wa habari alipokuwa akiitambulisha kamati  itakayoratibu mchezo huo.
Aidha mechi kama hizo zimekuwa zikiandaliwa kila baada ya kuahirishwa kwa Bunge na kuhusisha mpira wa miguu kati ya wabunge ambao ni wanachama na wapenzi wa timu ya Simba kwa upande mmoja na wale wa Yanga kwa upande mwingine.
“Mashindano yatakayofanyika mwaka huu ni kwa ajili ya kupata madawati mengi kadri itakavyowezekana kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kutatua kero ya upungufu wa madawati shule za msingi na sekondari nchini,” alifafanua Mhe. Ngeleja.
Mhe. Mgeleja aliendelea  kusema kuwa, ili kufanikisha mashindano hayo uongozi wa timu ya Bunge (Bunge Sports Club) umeunda kamati maalum ya maandalizi ili kufikia lengo lililokusudiwa kwa kuwatembelea na kuwahamasisha wadau mbalimbali Nchini Ili wachangie madawati.
Wabunge waliochaguliwa katika kamati hiyo ni Mwenyekiti Mhe. John Peter Kadutu (Ulyankulu), Makamu Mwenyekiti Mhe. Mussa Azzan Zungu (Ilala) pamoja na wajumbe Mhe. Salim Hassan Turky (Mpendae), Mhe. Ridhiwani Kikwete (Chalinze), Mhe. Mwigulu Nchemba (Iramba Magharibi), Mhe. Dkt. Dalaly Kafumu (Igunga).
Wajumbe wengine ni Mhe. Raphael Chegeni (Busega), Mhe. Mansoor Hiran (Kwimba), Mhe. Ahmed Shabiby (Gairo), Mhe. Bonna Kaluwa (Segerea), Mhe. Zaynab Vulu (Viti Maalum), Mhe. Abdul-Aziz Abood (Morogoro Mjini) na Mhe. Venance Mwamoto (Kilolo).
Aidha Mhe. Ngeleje amesema kwamba ameitambulisha kamati hiyo ili wadau waweze kuwatambua na kusiwe na maswali mara wajumbe hao wanapokutana na wadau kwa ajili ya kuwaomba kuchangia madawati  au fedha zitakazonunulia madawati na baadaye kukabidhiwa Serikalini ili yaweze kusambazwa Nchi nzima.
Vile vile amewaomba wadau ambao wako tayari kushirikiana na wabunge  katika uchangiaji wa madawati basi wasisite kuonana na kamati hiyo na kutoa michango yao.
Waratibu na waandaaji wa mashindano hayo ni Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na uongozi wa (Bunge Sports Club) ambapo mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa Ogasti 15, 2016

No comments:

Post a Comment