Siku mbili baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezi 18 gerezani kwa kosa la kumpiga teke dansa wake wa kike, Koffi Olomide ameachiwa huru na kurejea uraiani.
Taarifa ya Koffi kuachiwa huru imetolewa na promota wa Kenya aliyemwalika katika onyesho lililofanyika mwisho mwa wiki iliyopita, Jules Nsana ambaye alisema kuwa aliwasiliana na Koffi na kumweleza kuwa yupo nyumbani na familia yake.
“Nilizungumza na Olomide akiwa nyumbani kwake na akaniambia kuwa ameruhusiwa. Aikuwa na bendi yake, marafiki na familia . Ninafuraha na hilo,” alisema Nsana.
Koffi alitiwa katika mikono ya dola Julai, 26 akiwa nyumbani kwake na kuhumiwa kifungo cha miezi 18 gerezani kwa kosa la kumpiga mmoja wa madansa wake wa kike baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Jommo Kenyata nchini Kenya ambako alikuwa amekwenda kwa ajili ya kutumuiza katika onyesho.