KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

July 29, 2016

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI WATEKELEZA AGIZO LA RAIS KWA KUCHANGIA MADAWATI.

indexWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi  Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akimkabidhi  hundi Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya makabidhiano  madawati  ikiwa ni fedha zilizochangwa na watumishi wa wizara hiyo ikiwa sehemu ya kutekeleza agizo la Rais Mhe. John Magufuli  mapema hii leo katika shule ya Msingi Chamanzi iliyopo wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam . Picha na Beatrice Lyimo-MAELEZO
……………………………………………………………………………………………..
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Dar es salaam
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wamechangia kiasi cha Tsh. Milioni 100 ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha umma kuhusu zoezi la upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na Sekondari nchini.
Akikabidhi mchango huo kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kwa niaba ya watumishi wa wizara hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi  Augustine Mahiga amesema kuwa watumishi hao wametoa fedha hizo kwa shule ya msingi Chamazi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais la upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na sekondari nchini.
Balozi Mahiga amesema Wizara yake iliwahamasisha watumishi wake walio makao makuu na wale walio kwenye balozi mbalimbali nje ya nchi kuchangia zoezi hilo la upatikanaji wa madawati.
“Ili kufanisha upatikanaji wa fedha hizi Wizara yangu iliwahamasisha watumishi wake wote walio Makao makuu na wale walio katika balozi zetu duniani kote,  wito huu uliitikiwa kwa ari na hamasa kubwa na kufanikisha kukusanya kiasi cha Shilingi 100,176,825.52 za kitanzania”alisisitiza Balozi Mahiga
Waziri Mahiga aliongeza kuwa mara baada ya kukusanya fedha hizo watumishi wa Wizara hiyo waliamua kumpatia aliyekuwa Mtumishi wa Wizara ambaye sasa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni kiasi cha shilingi Milioni 15 kwa ajili ya ununuzi wa madawati katika Wilaya yake.
Aidha, amesema kiasi fedha zilizobaki zaidi ya shilingi milioni 85 zilikabidhiwa kwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa  kwa ajili ya mchango wa utengenezaji wa madawati ya shule ya Msingi Chamazi iliyoko Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
 
Waziri Mahiga aliongeza kuwa mbali na wizara yake kuwa na majukumu mbalimbali bado inalo jukumu la kuhakikisha inaitangaza Tanzania ili kuvutia wawekezaji na kukuza uchumi wa nchi, na kuongeza kuwa elimu bora ni msingi imara katika kufanikisha hilo.

No comments:

Post a Comment